Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 3 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

hii kama “nafsi tatu” ( hypostases ). (Nafsi ina akili timamu na kitovu tofauti cha fahamu. Nafsi hizi zinajua mambo mbalimbali na zinajua kwamba zinajua mambo hayo). Kwa hiyo, kuna Mungu mmoja anayeishi milele akiwa katika nafsi tatu. Huwezi kuelewa Maandiko au kueleza jinsi yanavyozungumza kuhusu Mungu ikiwa utajaribu kumwingiza Mwana ndani ya Baba au Roho au kinyume chake. Washirika wa Utatu wanawasiliana na kuitikiana katika uhusiano wa upendo. Na hatimaye kuna usawa. Kila mshirika wa Utatu ni Mungu sawa na mshirika mwingine. Kila mmoja wa washirika hawa anazo sifa za Mungu. Kila mmoja wa washirika hawa anapaswa kufikiriwa, na kuhusiana naye, kama Mungu. Kila mmoja wa washirika hawa anapaswa kuabudiwa na kuonyeshwa utii kama Mungu. Mwanatheolojia John Calvin anaongeza wazo la ziada katika hoja hii kwa kusema: “Wala Maandiko katika kuzungumza juu yake, hayajizuii kutumia jina “Mungu”. Paulo anadokeza kwamba sisi ni hekalu la Mungu, kutokana na ukweli kwamba ‘Roho wa Mungu anakaa ndani yetu’ (1 Kor. 3:16; 4:19; na 2 Kor. 4:16). Sasa, haipasi kupuuzwa hata kidogo, kwamba namna pekee ambayo ahadi zote ambazo Mungu anaziahidi za kutuchagua sisi kwa ajili yake kuwa hekalu lake, zimepata utimilifu wake kwa Roho wake anayekaa ndani yetu. Hakika, kama inavyoelezewa vizuri mno na Augustine (Ad Maximinum, waraka wa 66), ‘tungeamriwa kumjengea Roho hekalu la miti na mawe, maadamu ibada hiyo ni halali kwa Mungu peke yake, ungekuwa uthibitisho wa wazi wa uungu wa Roho; sasa ni uthibitisho ulio wazi zaidi kiasi gani kwamba hatupaswi kumjengea hekalu, bali kuwa sisi wenyewe ndio hekalu hilo.’ Na Mtume anasema wakati fulani kwamba sisi ni hekalu la Mungu, na wakati mwingine kwa maana hiyo hiyo, kwamba sisi tu hekalu la Roho Mtakatifu.” ~ Institutes. I.xii.15. Kuhusiana na dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu, Mwanathilojia Thomas C. Oden anaandika: Kufuru inayoongelewa hapa ni ile ya kuhusisha moja kwa moja nguvu za uovu na ujio wa Mungu katika historia kupitia Mwana na Roho (Marko. 3:28, 29 na kuendelea). Dhambi hii mara moja inamuweka mtu nje ya eneo ambalo msamaha unawezekana, kwa sababu

 8 Ukurasa 22 Kipengele II-C

 9 Ukurasa 24 Kipengele II-D

Made with FlippingBook - Share PDF online