Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 3 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

kila hatua kuelekea toba na imani inawezeshwa na Roho Mtakatifu. Kumkufuru Roho Mtakatifu ni kutojielewa kwa kiasi kikubwa kwa mtu binafsi mbele za uwepo wa Mungu. Maisha ya Paulo yanatoa ushahidi wa kutosha kwamba kufuru kama hiyo inaweza kusamehewa (1 Tim. 1:13). Kumkufuru Roho si jambo lisiloweza kusamehewa kwa maana ya kwamba Mungu hana uwezo na hataki kusamehe, lakini kwa maana ya kwamba mtenda dhambi hataki kupokea msamaha. Sio kwamba dhambi hiyo haiwezi kusamehewa kwa sababu kazi ya upatanisho ya Mwana haitoshi kwa dhambi hiyo, hapana, lakini kwa sababu kazi hiyo ya kutosha inabezwa kimakusudi, inazuiwa, na kuchukiwa na wale ambao kwao ingetosha kabisa (Ebr. 6:4-6). Dhambi hii inasemekana kuwa haiwezi kusamehewa kwa sababu maadamu tumedanganywa kiasi kwamba hatuwezi kutubu, hatuwezi kusamehewa, tukiwa tumefunga uwezekano wa kusamehewa kwa kujifungia sisi wenyewe mbali na Roho. Wale wenye hatia ya dhambi kama hizo wako katika mazingira ya aina hiyo na hawawezi kupokea msamaha. ~ Thomas C. Oden. Life in the Spirit: Systematic Theology toleo la 3. uk. 22. Katika hili tunapaswa kuongeza kwamba hakuna mtu anayeogopa kufanya dhambi hii isiyoweza kusamehewa, ambaye kuna uwezekano kwamba amewahi kuifanya. Kwa sababu ni utendaji kazi wa Roho peke yake katika maisha ambao humfanya mtu atambue dhambi na kuwa na wasiwasi kuhusu matokeo yake. Mtu ambaye amekataa kazi ya Roho bila kubadilika atapofushwa kiasi cha kutotambua kuwepo kwa dhambi yake mwenyewe na kutojali matokeo ya dhambi hiyo. Kwa Kiyunani, kama ilivyo kwa mfano, Kihispania au Kijerumani, kila nomino ni ya kiume, ya kike, au isiyo ya upande wowote. Nomino za kiume zinarejelewa kwa viwakilishi vya kiume, nomino za kike kwa viwakilishi vya kike, na nomino zisizo za upande wowote kwa viwakilishi visivyo vya upande wowote. Kwa hivyo, nomino zote zinaweza kuwa na viwakilishi vya yeye (Me), yeye(Ke) au hiki. Yohana 16:12, 14 - “Yeye (Me) atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote,”nk. Hapa, ingawa neno πνεύμα (pneuma), Roho, haliko upande wowote, neno εκείνος (ekeinos), Yeye (Me), ni la kiume; likikubaliana na Nafsi ya Uungu kuliko na neno lenyewe “Roho.” ~E. W. Bullinger. Figures of Speech Used in the Bible . Grand Rapids, MI: Baker, 1898 [Rpt. 1968]. uk. 701.

 10 Ukurasa 24 Ukurasa wa 22, kipengele II-E-1-b

Made with FlippingBook - Share PDF online