Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 3 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Wafafanuzi wengine wanadai kwamba kauli ya Yesu kwamba angekuja kwa wanafunzi wake ni ahadi kwamba angewatokea kimwili katika mwili wake wa baada ya kufufuka, wakati wengine wanaamini kwamba hii ni ahadi ya kumtuma Roho siku ya Pentekoste. Kwa maoni yetu, muktadha wa kifungu hicho cha Maandiko unaweka wazi kwamba Yesu anaahidi kuja kwao kwa njia ya kumtuma Roho wake. “Katika Injili hii, neno [ paraclete ] daima linatumiwa na Yesu, ambaye anazungumza juu ya Roho aliyetumwa kutimiza mahitaji ya wafuasi Wake baada ya kuondoka kwake.... Yafaa kutambua kwamba, kazi hizi zote zinazohusishwa na Roho mahali pengine katika Injili hii zinahusishwa na Kristo” ( Leon Morris, The Gospel According to John, New International Commentary on the New Testament, Grand Rapids, MI: Eerdmans, 1971 , ukurasa wa 663). Naye John Calvin anatoa maoni yake kwa usahihi kwamba: “Anaposema, nitakuja kwenu, anaonyesha jinsi anavyokaa ndani ya watu wake, na jinsi anavyovijaza vitu vyote. Ni, kwa uwezo wa Roho wake” ( Calvin’s Commentaries, Vol. XVIII, Grand Rapids, MI: Baker Book House, 1981, uk. 95). Uwiano huu kati ya uwepo wa Yesu (kimwili) na uwepo unaoendelea wa Roho Mtakatifu ni sawa na kusema kwamba kuishi maisha ya ufuasi mbele za Mungu kunaweza kuelezewa kama “kutembea katika nyayo za Yesu” au “kutembea kwa Roho.” 1 Yohana 2:6 - Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda [ p ě ripat ěō] mwenyewe vilevile kama yeye alivyoenenda. Wagalatia 5:16 - Basi nasema, enendeni [ p ě ripat ěō] kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kuenenda kama Yesu na kutembea kwa kuongozwa na Roho, kibiblia, ni jambo lilelile. Na ni Roho Mtakatifu mwenyewe ambaye huja kuwa “pamoja nasi” kutusaidia kuenenda kama Yesu alivyoenenda. Mwanatheolojia Michael Green anasisitiza kwa usahihi kwamba tofauti kuu kati ya maelezo ya Agano la Kale na maelezo ya Agano Jipya kuhusu Roho ni kwamba Roho anachukua huduma ya kumwakilisha Kristo. Anaandika: Roho Mtakatifu hajulikani tena kama nguvu tupu; amevikwa nafsi na tabia ya Yesu. Kwa maana nyingine, Yesu ndiye “bomba” ambalo kupitia kwake Roho hupatikana kwa wanadamu. Yesu anamweka Roho katika nafasi kamili ya nafsi. Yesu ndiye mche
11 Ukurasa 25 Kipengele II-E-2-b
12 Ukurasa 25 Kipengele II-E-2-c
Made with FlippingBook - Share PDF online