Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 3 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

ambao kupitia kwake nuru ya Roho iliyosambazwa na kuwaka inahifadhiwa. Yesu ndiye nabii (Luka 7:16, Mdo. 3:22, 7:37) wa nyakati za mwisho, ambaye kupitia kwake Roho wa unabii, aliyefanya kazi sana katika Agano la Kale, alitoa ufunuo kamili na wa mwisho. . . . Yesu alimtoa Roho huyu kwa wanafunzi wake kwa msingi na kufuatia kifo na ufufuo wake. Kinachofuata ni kwamba Roho atahusishwa na tabia ya Yesu milele. . . . [Yohana 16:7 linatufundisha hivyo] ni kazi ya Msaidizi kufanya uwepo wa Yesu uenee ulimwenguni kote. Katika siku zake akiwa katika mwili, Yesu aliwekewa mipaka na nafasi na wakati. Kuondoka kwake kimwili kuliwezesha ujio wa Roho kama Msaidizi na hakungekuwa na vizuizi vya nafasi na wakati kuzuia wanafunzi kuwa katika uhusiano wa karibu naye.

~ Michael Green. I Believe in the Holy Spirit . Grand Rapids: Eerdmans, 1989. kurasa za 47-48.

Mtazamo kuhusu Roho unaompunguza mpaka kwenye sitiari ya nguvu za Mungu hauwezi kamwe kuutendea haki mtazamo wa Agano Jipya kwamba Roho anafanya kazi kama uwepo na sauti hai ya Yesu katika mioyo ya watu wa Mungu.

Mtakatifu Basil anaonyesha kwamba kitendo cha kuwa mwombezi katika maombi, kitu ambacho ni ushahidi wa hali yake ya kuwa nafsi, kisichukuliwe kama hoja dhidi ya uungu wake. Anasema: [Wapinzani wetu wanaoji] Lakini inasemekana kwamba “Yeye anatuombea.” Kisha inafuata hoja kwamba, kama vile ilivyo kwamba mwombaji ni mdogo kwa mfadhili, vivyo hivyo na Roho ni mdogo katika hadhi kwa Mungu. Lakini je, hujawahi kusikia kuhusu Mwana wa Pekee kwamba “yuko upande wa kuume wa Mungu, ambaye pia hutuombea”? Basi, kwa sababu Roho yu ndani yako,. . . kwa sababu hii usijiruhusu kujikosesha mtazamo sahihi na mtakatifu kumuhusu yeye.Kwa maana kufanya fadhili zenye upendo za mfadhili wako kuwa msingi wa kutokuwa na shukrani kwa hakika kulikuwa ni kutotenda haki kulikopita kiasi. ~ On the Holy Spirit (De Spiritu Sancto)

 13 Ukurasa 26 Kipengele II-E-3-e

Made with FlippingBook - Share PDF online