Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 3 5

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Mtakatifu Augustino anatoa mtazamo wa kawaida wa Magharibi (Katoliki na Kiprotestanti) wa Yohana 15:26 anapoandika: Ikiwa, basi, Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na kwa Mwana, kwa nini Mwana alisema, “Anatoka kwa Baba?” Mnadhani ni kwanini, ikiwa si tu kwamba kama alivyozoea kumrejelea, ndivyo pia asemavyo, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali ni yake yeye aliyenituma”? Basi, ikiwa ni mafundisho yake yanayoongelewa hapa, ambayo Yeye alisema hayakuwa yake mwenyewe, bali ya yeye aliyemtuma, ni kwa kiasi gani zaidi tunaweza kuelewa kwamba Roho naye ametoka kwake mwenyewe, pale asemapo Atoka kwa Baba, kana kwamba hasemi, Yeye hatoki kwangu? Hakika ametoka kwake, kutoka kwa Yeye ambaye Mwana alipewa asili yake ya Uungu, kwa maana Yeye ni Mungu wa Mungu, pia anayo sifa hiyo ya kumtoa Roho Mtakatifu; na kwa hiyo Roho Mtakatifu amepokea kutoka kwa Baba mwenyewe, kwamba anapaswa kutoka kwa Mwana pia, kama tu atokavyo kwa Baba. ~ Imenukuliwa katika, ed. The Holy Spirit: Ancient Christian Traditions . Peabody, MA: Hendrickson, 1984. uk. 183. Baadhi ya wanatheolojia waKikatoliki, Kiothodoksi, naKiprotestanti wamedokeza kwamba mjadala juu ya kifungu cha filioque katika Kanuni ya Imani ungeweza kusuluhishwa kwa maneno, “ambaye hutoka kwa Baba kupitia Mwana.” Kanuni hii ilipatikana mapema nyakati za Mt. Basil na ilipendekezwa kama suluhisho la Kiekumene na Mtaguso wa Florence katika Mwaka 1439 B. K Ingawa bado haijaanza kutumiwa rasmi na kanisa lolote kama Tamko la imani, hivyo inabaki kuwa sehemu ya mijadala ya sasa ya Kiekumene juu ya mada hii. Kama hatukubali mchakato wa aina mbili wa kutolewa kwa Roho, hakutakuwa na mwanga juu ya namna ya kutofautisha kati ya Mwana na Roho. Washiriki wote watatu ni wa milele, wako sawa, na wanasifa za kuwa na nguvu zote, kujua mambo yote na kuwepo kila mahali. Ni nini basi kinachowatofautisha? Tunatofautisha kati ya Baba na Mwana kwa sababu mmoja ametokana na mwingine – yaani, asili ya mmoja inatokana na asili ya mwingine. Lakini tukisema kwamba Mwana atoka kwa Baba pekee na kwamba Roho atoka kwa Baba pekee – kuna tofauti gani

 14 Ukurasa 27 Kipengele III-A-1

 15 Ukurasa 28 Kipengele III-A-2-c

 16 Ukurasa 28 Kipengele III-A-2-d

Made with FlippingBook - Share PDF online