Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 3 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

kati ya Mwana na Roho? Kanisa la Magharibi linasema tofauti ni kwamba Roho anatoka kwa Baba na kwa Mwana . Roho anatokana na upendo baina yao wawili. “Udhihirisho” – hili lipo karibu sana na moja ya mambo makuu ambayo yanahusishwa na “Utolewaji.” Utukufu wa milele, jumuiko la pendo changamfu, kujitoa kwa siri ya ndani kabisa, mlipuko wa usahili safi, furaha ijayo isiyo na ukomo wa wakati.... Katika kila moja ya viwango hivi Roho ndiye nguvu na msukumo, uwepo wenye ufanisi, wa Mungu kupenda kuwa na kutenda kwa ajili ya mwingine. ~ David Willis. Clues to the Nicene Creed: A Brief Outline of the Faith . Grand Rapids: Eerdmans, 2005. uk. 128. Ni muhimu kwamba tafsiri ya Mt. Augustine kuhusu Roho kama “Upendo Wenyewe” au “kifungo cha Upendo” isieleweke kwa namna ya kuficha nafsi ya Roho Mtakatifu. Mawazo yetu ni dhaifu kweli linapokuja suala la uwepo wa Utatu. Hata taswira hii ya “kifungo cha upendo” inakosa kuhusisha kikamilifu suala la kwamba Roho ni nafsi, huku ikiacha dhana ya uwezekano wa Washirika wawili (uwili), yaani Baba na Mwana pamoja na kifungo hicho, badala ya kuleta wazo la Utatu. Inaweza kumpunguza Roho katika mazingira ya kuukuza upendo. Roho ni zaidi ya hivyo, hata hivyo, yeye ni nafsi tofauti ambaye mbali na kuwaunganisha wengine katika upendo, bado yeye mwenyewe anashiriki na kuhusika katika huo.... Ingawa tunapendezwa na mfano wa kifungo cha upendo, hatutaki kukosa kutenda haki kwa usawaziko wa kweli wa Utatu au kuacha wazo la kifungo ambacho si nafsi na ambacho kingeweza kuficha ukweli kwamba Roho ni nafsi. ~ Clark H. Pinnock. Flame of Love: A Theology of the Holy Spirit . Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1996. uk. 40. Kwa ufahamu zaidi juu ya mtazamo wa Mt. Augustino kuhusiana na Roho Mtakatifu tazama kitabu cha “On the Holy Trinity,” Nicene and Post-Nicene Fathers, First Series, Vol. 3.

 17 Ukurasa 30 Kipengele III-B-4-c

Made with FlippingBook - Share PDF online