Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 3 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Maisha ya ndani ya Utatu ni siri kuu. Nukuu ya Clark Pinnock inafuatia mapokeo yaliyoheshimiwa wakati fulani katika theolojia kwa kurejelea maisha ya ndani ya Mungu kama “Dansi ya upendo.” Neno la kithelojia kwa ajili ya hili ni perichoresis ( peri–mduara , choresis -mchezo). Mt. Yohana wa Dameski alitumia neno hili kuelezea uhusiano uliopo kati ya Baba, Mwana na Roho. Fundisho la perichoresis linadai kwamba kila mmoja katika Nafsi tatu anashiriki uzima wa wenzake na anaishi ndani ya wenzake, na bado anabaki tofauti na wenzake. [Kwa mfano, Yesu anasema “Mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu”(Yohana 14:10, linganisha na Yohana 10:38) na “Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba” (Yohana 14.9) na bado kwa wakati huohuo yeye ametumwa na Baba ulimwenguni, kuwa mtii kwa mapenzi ya Baba, na kurudi tena kwake na kukaa mkono wa kuume wa Baba]. Washirika hawa wa Utatu wanakaa na kujidhatiti kila mmoja ndani ya mwingine. Kwa maana hawagawanyiki na hawawezi kutengana, bali wameshikamana, pasipo kuungana au kuchanganyikana, huku wakishikamana kila moja na mwingine. Kwa maana Mwana yu ndani ya Baba na Roho: na Roho ndani ya Baba na Mwana: na Baba ndani ya Mwana na Roho, lakini hawaungani wala kuchanganyika. ~ St. John of Damascus. Nicene and Post-Nicene Fathers , Series 2. “Exposition of the Orthodox Faith,” 1.14. Hivyo umoja na utofauti wa uhusiano katika Utatu unaelezewa kwa usahihi kama “Dansi ya Kiungu ya Upendo” na ufahamu wa Augustino kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu kama “kifungo cha upendo” unauongezea nguvu mlinganisho huu. Utetezi wa msingi wa mafundisho ya kumwabudu na kumtukuza Roho wa Mungu unapatikana katika kitabu cha On the Holy Spirit cha Mtakatifu Basil (329-379 B.K). Mwanatheolojia Millard J. Erickson katika kitabu chake cha, God in Three Person: A Contemporary Interpretation of the Trinity, [yaani Mungu katika Nafsi Tatu: Tafsiri ya Kisasa ya Utatu ], anatukumbusha kwamba swali kuhusu ibada ya Roho Mtakatifu ni sehemu ya swali kubwa la Utatu: Je tunatakiwa kumwomba na kumwabudu Baba peke yake? Au maombi yote na ibada vinatakiwa kwenda moja kwa moja kwa Mungu mmoja aliye katika Nafsi Tatu (bila kujali ni Nafsi ipi inalengwa)? Mapema sana, Kanisa lilifikia hitimisho kwamba Maandilo yameelekeza kumwabudu Yesu

 18 Ukurasa 30 Kipengele III-B-5

 19 Ukurasa 31 Kipengele IV-A

Made with FlippingBook - Share PDF online