Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 3 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

kama Bwana (Mt. 21:15-16; Yoh. 20:28; Ufu. 1:5-6, 5:8-14) na kuomba kwake (Mdo 7:59; Rum. 10:13; 1 Kor. 1:2). Kwa kuwa Yesu amempeleka Roho Mtakatifu kwetu kuwa “Msaidizi mwingine” kama Yeye na kwa kuwa ni utendaji wa Roho Mtakatifu tu unaotuwezesha kufanya ibada ya kweli (1 Kor. 12:3) na maombi (Rum. 8:26), basi Kanisa liliona hiyo kama sababu kwamba maombi na ibada kwa Roho Mtakatifu ilikuwa ni mwitikio wa kawaida kwa lile jukumu lake la “kuja kuwa pamoja nasi” ili kufanyika uwepo wa Kristo katika maisha yetu. Hatimaye, Theolojia ya Kikristo imeshawishika kwamba umoja wa Utatu unataka kwamba tusitenganishe ibada yetu bali tuitikie kwa Mungu katika utimilifu wake kwa sifa, ibada na kicho cha heshima. “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu! Mwenye rehema na nguvu; Mungu katika Nafsi Tatu, Utatu uliobarikiwa.”

Wimbo Come Thou Almighty King (Uje Wewe Mfalme Mwenyezi) ni mfano mzuri wa tenzi ambazo ubeti wa kwanza unalenga kumwabudu Mungu Baba, ubeti wa pili kumwabudu Mwana, ubeti wa tatu kumwabudu Mungu Roho Mtakatifu, na ubeti wa mwisho unaelekeza ibada kwa Mungu mmoja katika Utatu Mtakatifu.

 20 Ukurasa 32 Kipengele IV-B-3

Uje Wewe Mfalme Mwenyezi Maandishi: Hajulikani/Muziki: Felice de Giardini, 1716-1796

Uje, wewe Mfalme mwenyezi, Tusaidie kuliimbia jina lako, tusaidie kusifu!

Baba mtukufu, mshindi wa vyote, Uje utawale juu yetu, Mzee wa Siku!

Uje, wewe Neno uliyefanyika mwili, Jifunge upanga wako wenye nguvu, sikia maombi yetu! Uje, na uwabariki watu wako, na kulifanikisha Neno lako; Roho wa utakatifu, shuka juu yetu!

Uje, Mfariji mtakatifu, Ushahidi wako mtakatifu utoe katika saa hii ya furaha.

Made with FlippingBook - Share PDF online