Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 4 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
na matendo yake, kama matawi ya mzabibu. Tunamtambua Yesu na kumwitikia kwa imani kupitia kazi ya Roho Mtakatifu anaye tuangazia, na tunamtambua Roho na kumwitikia kwa sababu anamwakilisha Kristo na mafundisho yake kwa uaminifu.
Katika kipindi hiki cha ufunguzi ni muhimu sana uanze kujenga uhusiano na wanafunzi wako. Waonyeshe kwamba unawajali kibinafsi na unajali wito wao wa huduma. Wao sio tu “wanafunzi” bali ni viongozi wa Kanisa. Wanapaswa kuona kwamba unaliona darasa hili, si tu kama ni kwa ajili ya mazoezi ya kitaaluma, bali kama njia ya kuwatayarisha ili kulijenga Kanisa na kutimiza makusudi ya Mungu. Wahimize wanafunzi darasani kuwashirikisha wengine hali halisi wanazokabiliana nazo katika huduma wiki hii na tumia muda kuwaombea na kutiana moyo. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa zoezi la wiki ijayo, hasa lile la kuandisha muhtasari wa vitabu utakavyo waelekeza kusoma. Hili sio gumu; lengo ni kwamba wasome vitabu hivyo kwa kadiri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile ambacho wanaamini waandishi walimaanisha. Huu ni ujuzi muhimu wa kiakili kwa wanafunzi wako kujifunza, kwa hivyo hakikisha kwamba unawatia moyo katika mchakato huu. Na kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kuliona hili kuwa gumu, wahakikishie kuhusu dhamira ya zoezi hili, na uwasisitizie kwamba uelewa wao wa maelezo hayo ndio muhimu zaidi, si ujuzi wao wa kuandika. Ni kweli, tunataka kuboresha ujuzi wao, lakini si katika namna inayo dhoofisha lengo la kuwatia moyo na kuwajenga. Hata hivyo, hatutaki wafanye chini ya kiwango cha ubora wanachotakiwa kufanya. Jitahidi kutafuta mbinu zenye uwiano mzuri kati ya kuwapa changamoto ya kufanya kwa ubora na kuhakikisha hawavunjiki moyo.
30 Ukurasa 46 Ushauri na Maombi
31 Ukurasa 47 Kazi
Made with FlippingBook - Share PDF online