Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
2 4 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
kada ya masuala kadha wa kadha, mashaka, maswali, na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na uzoefu wao, kisha husianisha hayo na maisha na huduma zao. Usisite kutumia muda mwingi kwa ajili swali fulani lililotokana na video, au jambo maalum ambalo linafaa hasa katika muktadha wa huduma wanazofanya wakati huu. Lengo la sehemu hii ni kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine, maswali yaliyo hapa chini yametolewa kama miongozo na vichochezi tu, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chagua na uchukue kutoka katika hayo, au uje na maswali yako mwenyewe. Jambo la muhimu ni tija ya maswali hayo sasa, kwa muktadha wao na kwa maswali yao. Kushughulika na mafundisho ya uongo ya makundi ya Kikristo yenye imani potofu ni kipengele nyeti sana katika elimu ya theolojia ya Kikristo. Lengo la kifani hiki ni kuangalia na kuona kama wanafunzi wako wanaweza kutetea fundisho la Nafsi ya Roho Mtakatifu kwa maneno yao wenyewe kwa kutumia Maandiko. Hili ni muhimu kulifanya kwa sababu karibu kila kiongozi wa Kikristo atalazimika kufanya hivi wakati fulani katika huduma yake. Wanafunzi wanapopitia majibu yao, wakumbushe kwamba kuna mambo mawili ambayo kiongozi hasa wa kazi za kichungaji lazima ajibu. Kwanza, anapaswa kujibu yaliyomo katika nukuu au hoja iliyojengwa, anapaswa kusahihisha na kukanusha mafundisho ya uongo. Lakini pili, lazima pia kumjibu mtu aliyeleta hoja. Sue anapaswa kujibiwa kwa sauti gani? Je, yeye ni “mbwa-mwitu mkali” (Mdo 20:29; 2 Yoh. 10-11) anayejaribu kudhoofisha kundi kimakusudi? Au, yeye ni mtafutaji mpotovu na aliyechanganyikiwa anayehitaji mafundisho na matunzo ya kichungaji (2 Tim. 2:24-26)? Jambo muhimu zaidi kuhusu kifani hiki ni kwa wanafunzi kutambua nguvu ya kauli ya Yesu katika Yohana 14:16 kwamba anamtuma Roho Mtakatifu kuwa “Msaidizi mwingine [ paraclete ].” RohoMtakatifu daima anawakilisha na kutenda kwa uaminifu mahali pa Kristo kwa ajili yetu. Kama vile Yesu alivyoweza kudai kwamba mtu yeyote aliyekuwa amemwona yeye alikuwa amemwona Baba (Yohana 14:9), ni kweli vile vile kwamba mtu yeyote ambaye amemwona Yesu atamtambua Roho ambaye yeye amemtuma. Kukaa kwa Roho ndani yetu kunatuunganisha na Kristo Aliye Hai ili kwamba tuunganishwe katika upendo wake, nia yake, maneno yake,
28 Ukurasa 44 Uchunguzi Kifani no.1
29 Ukurasa 45 Uchunguzi Kifani no.2
Made with FlippingBook - Share PDF online