Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 4 1
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Umbo lililozoeleka zaidi la taswira ya hua katika Biblia linaonekana kwenye simulizi za ubatizo ambapo Roho wa Mungu anashuka kutoka mbinguni “kama hua” (Mt. 3:16)... Hata hivyo inambidi mtu afikirie kuhusu kitabu cha Mwanzo 1:2, ambapo Roho wa Mungu, maji, pamoja na mfano wa ndege vinaonekana tena (m e rahepet = “jongea” au “elea” ni taswira ya ndege, taz. Kumbukumbu la Torati 32:11). Katika Talmud (b. Hag. 15a) inafananisha kuelea kwa Roho juu ya maji wakati wa uumbaji na kupepea kwa njiwa, na pia 4!521, kipande cha Hati-kunjo ya Bahari ya Chumvi [Dead Sea Scroll], kinakipa kitabu cha Mwanzo 1:2 matumizi mengine ya kieskatolojia: Roho ataelea juu ya watakatifu katika siku za mwisho. Kwa hiyo njiwa wakati wa ubatizo anaonekana kuwa na maana kwamba Yesu analeta uumbaji mpya. ~Leland Ryken, James C. Wilhoit and Tremper Longman III, Gen. ed. “Dove.” Dictionary of Biblical Imagery . Downers Grove, IL/Leicester, England: InterVarsity Press, 1998. uk. 217. Wasidie wanafunzi kuona kwamba huduma nzima ya Roho Mtakatifu ina dhumuni na kusudi lililokubwa zaidi la siku za mwisho. Kusudi la Mungu ni mbingu mpya na nchi mpya, inayokaliwa na jamii mpya ya wanadamu (Kanisa), na kuunganishwa katika amani kamilifu chini ya utawala wa Kristo. Roho sio tu anautegemeza ulimwengu wa sasa, lakini pia anafanya kazi kwa bidii ili kutimiza kusudi kuu la Mungu la uumbaji mpya. Zilizoorodheshwa hapa chini ni kweli za msingi zilizoandikwa katika mfumo wa sentesi ambazo wanafunzi wanatakiwa kuwa wamezipokea kutoka kwenye somo hili, ikimaanisha kutoka kwenye video walizotazama na mijadala waliyoifanya chini ya uongozi wako. Hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa vizuri na zimewekewa mkazo kwa umakini mkubwa, kwasababu, kazi zao za majaribio na mitihani zitachukuliwa kutoka kwenye dhana hizo moja kwa moja.
24 Ukurasa 39 Kipengele III-B-2-d
25 Ukurasa 41 Hitimisho
26 Ukurasa 42 Muhtasari wa Dhana Kuu
Katika kuwasaidia wanafunzi wako kufikiria hali zao wenyewe, unaweza kubuni baadhi ya maswali au kutumia yale yaliyotolewa hapa chini kama tu njia ya kuchochea shauku yao. Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, lakini ni kwako wewe, katika mazungumzo na wanafunzi wako, kutatua
27 Ukurasa 43 Kutendea kazi somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook - Share PDF online