Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 4 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

James Version na New King James Version] . Linganisha “roho ya neema na kuomba” na “Roho ya…..” • Ezekieli 37:9 Katika matoleo ya Maandiko ya English Standard Version , the New American Standard (NASB ), na the New English Bible (NEB). Humo zingatia maana rejea za neno Roho: “pumzi,” “roho,” na “upepo.” Ezekieli 37:9 – Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. JohnCalvin anafuata nyayozawanatheolojiawa kalewaKanisa katika kuwatofautisha washirika wa Utatu kwa njia hii: Tofauti hii ni kwamba, Baba anahusishwa na mwanzo wa utendaji, chemchemi na chanzo cha vitu vyote; Mwana anahusishwa na hekima na shauri, na mpangilio katika utendaji, huku nguvu na ufanisi wa utendaji vikihusishwa na Roho [msisitizo ni wangu]. ~ Institutes, I.xiii.18. Wakati nafsi zote tatu kimsingi zinatenda katika umoja katika kila tendo linalotendwa na Mungu, tunaweza kumzungumzia Mungu Baba kuwa ndiye msingi wa kila tendo, Mungu Mwana (Logos) akiwa ndiye mpangiliaji wa kila tendo, na Mungu Roho ni mtekelezaji anayetimiliza kila tendo kwa nguvu. Hivyo mtazamo wa Agano la Kale juu ya Roho Mtakatifu kama nguvu ya Mungu katika utendaji unaendana kabisa na kazi ya Roho inayopatikana katika theolojia ya Agano Jipya ya Mungu katika Utatu. KUMBUKA: Tunapozungumzia kazi za kila nafsi katika Utatu tunaongea kuhusu “fundisho la iktisadi ya Utatu” (yaani namna ambavyo Baba, Mwana na Roho wanafanya kazi kuhusiana na uumbaji wao) hii ikiwa kinyume na “fundisho la kiontolojia la Utatu ” (yaani namna ambavyo Baba, Mwana, na Roho wanaendelea kuwepo—ikiwa na maana kwamba Baba mara zote anatoa [anazalisha], Mwana anatolewa, na Roho mara zote anatoka kwao).

 23 Ukurasa 35 Kipengele II-B-2

Made with FlippingBook - Share PDF online