Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 4 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu
MAELEZO YA MKUFUNZI 2
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 2, Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu. Lengo la jumla la moduli ya Mungu Roho Mtakatifu ni kuwawezesha wanafunzi wako kumwelewa Roho Mtakatifu ni nani (nafsi) na kile anachofanya (kazi), kuweza kutetea ufahamu huu kwa kutumia Maandiko, na kuona maana ya kweli hizi katika huduma ndani ya kanisa na kupitia kanisa. Lengo la somo hili ni kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba ujuzi wowote wa Mungu huja kupitia huduma ya Roho Mtakatifu. Roho wa Mungu ndiye anayemfunua Mungu kwa njia ya maneno ya kinabii na pia ndiye anayewawezesha wanadamu kukombolewa kutoka katika upofu wa kiroho ili waweze kuelewa na kuitikia ukweli kuhusu Mungu. Katika somo hili lote unapaswa kujaribu kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa na kuepuka uzushi wa Pelagio (tazama maelezo ya mkufunzi kwa ajili ya Sehemu ya pili) ambao unafundisha kwa uongo kwamba mwanadamu wa asili anaweza kumwelewa Mungu na kuitikia kwake pasipo msaada wa neema na nguvu kutoka kwa Roho Mtakatifu. Tafadhali zingatia tena kwamba kweli hizi zimeelezewa kwa uwazi katika malengo ya somo. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na muda wako wa kukaa na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kukazia malengo haya katika kipindi chote darasani, ndivyo unavyozidi kuongeza uwezekano wa wanafunzi kuyaelewa na kuona namna yalivyo muhimu. Mkazo wa ibada hii ni juu ya kipawa au karama ya Maandiko ambayo “yalivuviwa” na Roho Mtakatifu kupitia manabii. Mara nyingi tunazungumza juu ya “karama za Roho” kwa maana pekee ya charismata, yaani namna za uwezeshaji maalum ambazo analipa Kanisa kwa ajili ya huduma. Wakati katika maana halisi, kila mtu katika darasa hili ambaye ana Biblia huyo pia ana “karama ya Roho.” Neno la Mungu lenyewe tu, ni kipawa kikuu cha Roho kwa wanadamu. Bila ufunuo huu wa kiungu jamii nzima ya wanadamu ingepotea isiweze kumtambua Mungu aliye Hai wala makusudi yake. Kila kitu unachofundisha katika kozi hii kuhusu Mungu kitawezekana tu kwa sababu ya ukweli kwamba “watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” Ni hazina ya ajabu namna gani tuliyo
1 Ukurasa 51 Utangulizi wa somo
2 Ukurasa 52 Ibada
Made with FlippingBook - Share PDF online