Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 4 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

nayo katika Maandiko Matakatifu na ni deni kiasi gani tulilo nalo kwa Roho wa neema wa Mungu ambaye humfunua Mungu Aliye Hai kwetu. KUMBUKA: Athenagora, ambaye amenukuliwa katika kipengele cha ibada, alikuwa mwanafalsafa wa Athene ambaye aligeukia Ukristo na aliandika kazi zake mbili miaka ya 177 B.K ambazo bado zip, nazo ni “A Plea for Christians” [Ombi kwa Wakristo] na “Treatise on the Resurrection of the Dead” [Tasnifu juu ya Ufufuo wa Wafu], ambazo zote zinaweza kupatikana katika kitabu cha The Ante-Nicene Fathers [Mababa wa Kabla ya Nikea], Toleo la 2. Linapokuja suala la kumjua Mungu, hatua ya kwanza iko upande wake. Asipojifunua, hakuna unachoweza kufanya kitakachokuwezesha kumfahamu. ~ C. S. Lewis. Mere Christianity . Wakristo wanakiri kujua kuhusu Mungu, si kupitia sayansi, falsafa, au sanaa fulani bali kupitia “maneno ya kinabii” yaliyovuviwa na Roho. Tunachojua kuhusu Mungu hutujia kupitia ufunuo badala ya jitihada za kibinadamu. [Mwanatheolojia Karl Barth yuko sahihi katika hoja hii, shimo kati ya Mungu na mwanadamu ni pana sana kiasi kwamba haliwezi kuunganishwa kutokea upande wa mwanadamu]. Mungu huchukua hatua ya kujidhihirisha kwetu. Kulingana na 1 Kor. 2:10-12, Roho huchunguza mambo mazito ya Mungu na sio tu kuweka ujuzi huu katika maneno aliyoyachagua mwenyewe bali humjaza mwamini ufahamu unaoyafanya maneno hayo (ambayo bila hayo, maneno ya kibinadamu yasingetosha kumwelezea Mungu asiye na mwisho) kuwa yenye kueleweka na yenye maana. Baadaye katika somo hili tutarejelea kazi hii ya aina mbili ya Roho kama kuvuvia na kuanganzia (kutia nuru). Ufunuo wa jumla (uumbaji na ujuzi wa Mungu uliowekwa katika moyo wa mwanadamu) nyakati fulani unaweza kuwasadikisha watu kwamba Mungu yuko, lakini ni ufunuo wa Mungu pekee kupitia Mwana wake na kupitia Roho wake unaoweza kuwawezesha watu kumjua yeye kwa uhalisia jinsi alivyo, na mapenzi na makusudi yake mahusui kwa wanadamu. Kumbuka: Theolojia ya Kikatoliki imekuwa tayari kutoa jukumu kubwa zaidi kwa “Ufunuo wa Jumla” (na Theolojia ya Asili ambayo inaweza kutokana nayo) kuliko Waprotestanti wengi. (Angalia “Theolojia Asilia” katika Kamusi ya Kiinjili ya

 3 Ukurasa 53 Kujenga Daraja – Sehemu ya 1

Made with FlippingBook - Share PDF online