Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 4 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Theolojia, Walter A. Elwell, ed. Grand Rapids, MI: Baker, 1984, kwa makala nzuri ya utangulizi kuhusu mjadala huu).

Ruhusuwanafunzi wachachewalieleze kundi zima njia ambazoRoho aliwashuhudia kwa habari ya dhambi. (Kwa kuwa ushuhuda mzima wa wokovu wa watu wakati mwingine unaweza kuwa mrefu, unaweza kuwaelekeza wale wanaoeleza kujikita katika mada mahususi - i.e. jinsi ambavyo Roho aliwafanya waamini kwamba wanamwitaji Mungu). Baada ya muda wa zoezi hilo kukamilika, zungumza maneno haya: “Roho Mtakatifu daima anafanya kazi ulimwenguni kuwafanya watu watambue hitaji lao la kupatanishwa na Mungu. Huu ulikuwa ujumbe mkuu wakati wowote Roho ‘alipozungumza kupitia manabii.’ Leo tutaenda kuangazia njia ambazo Roho huifunua Kweli kinabii na kuwaita watu kuiamini na kuitii”. Unabii unaweza kufafanuliwa kama njia ya kujua ukweli; na kwa hivyo, unaweza kulinganishwa na kutofautishwa na falsafa. Katika udhihirisho wake wa kibiblia unabii unaunda sehemu ya theolojia ya Roho Mtakatifu na unawakilishwa kama njia moja ya ufunuo wa kiungu wa ukweli wa Mungu au, kwa maana pana zaidi, ndio jumla ya ufunuo huo.... Kama falsafa, unabii unalenga kutoa ukweli kuhusu Mungu, mwanadamu na ulimwengu.... Utofauti wake na falsafa ni kwamba, mahali pa kuanzia ni Mungu na chanzo chake cha maarifa ni ufunuo wa kimungu –ukweli uliopokelewa, badala ya ukweli unaopatikana kwa sababu za kibinadamu au uzoefu. ~ “Prophecy.” New Dictionary of Theology . uk. 537. Nabii mara zote ni Mtu aliyesikia kutoka kwa Mungu na ambaye ujumbe wake unawakilisha nia ya Mungu inayozungumzwa kwa njia ya Roho Mtakatifu. Torati imeundwa na Vitabu Vitano vya Musa, Vitabu vya Manabii vimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni “Manabii ya Mwanzo” (Yoshua, Waamuzi, Samweli naWafalme), “Manabii waMwisho” (Isaya, Yeremia, Ezekieli), na “Kitabu cha Manabii Kumi na Mbili,” na vitabu vya Maandishi mengine vinahusisha Zaburi, Mithali, Ayubu, Uwimbo Ulio Bora, Ruthi, Maombolezo, Mhubiri, Esta, Danieli, Ezra, Nehemia na Mambo ya Nyakati.

 4 Ukurasa 54 Kujenga Daraja – Sehemu ya 2.

 5 Ukurasa 56 Kipengele I-A

 6 Ukurasa 57 Kipengele I-B-2-a

Made with FlippingBook - Share PDF online