Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
2 4 8 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Maandiko ndiyo kilele cha kazi ya kinabii ya Roho Mtakatifu. Kanoni ya Maandiko (Biblia) ni ushahidi wa kipekee wa kinabii kuhusu Mungu na makusudi yake ambayo yamekusudiwa kwa watu wote nyakati zote na mahali pote. [Unabii] ulipewa mamlaka isiyotiliwa shaka baada tu ya kuhakikiwa (rej. 1 The. 5:19-21). Hata pale ulipotambulika kuwa ni neno la kimungu, bado haikutosha kuwa neno la kikanuni [au kuwa sehemu ya Biblia]. Unabii ulikuwa na (na una) matumizi muhimu sana kwa walengwa wake wa kwanza lakini ulipewa hadhi ya kikanuni pale tu ulipotambuliwa pia kama ufunuo wenye mamlaka unaoweza kutumika pia kwa vizazi vijavyo na kipimo thabiti kwa ajili ya kupima na kuthibitisha unabii wa wa nyakati za baadaye. ~ E. E. Ellis. “Prophecy, Theology of.” New Dictionary of Theology . Sinclair Ferguson, David F. Wright, and J. I. Packer, eds. Downers Grove, IL/Leicester, England: InterVarsity Press, 1988. uk. 538. Kitendo cha Roho kuvuvia Maandiko ndio njia muhimu sana ambayo kwayo “aliongea kupitia Manabii.” Na ndio neno pekee la kinabii ambalo linaweza kutumika kwa mamlaka kamili kupima madai ya wale wanaodai kupokea neno kutoka kwa Roho kwa ajili ya Kanisa leo. Kwa ujumla, kazi ya kutia nuru ni ile kazi ya ndani ya mtu ambayo Roho Mtakatifu anaifanya kuangaza akili na moyo wa mtu anayesikia Neno. Wafafanuzi wengi wanaongezea kwamba Roho sio tu anaangazia moja kwa moja kwa kuzungumza na moyo na akili ya msikilizaji lakini pia anatoa kipawa cha kufundisha kwa viongozi katika Kanisa. Huduma ya kuhubiri na kufundisha inaangazia maana za Maandiko kwa wale wanaoyasikia. Kwa hiyo, kwa mfano, Filipo alipoelezea maana ya Maandiko kwa towashi Mwithiopia, Roho aliangazia Maandiko kupitia kipawa cha kufundisha alichompa Filipo. Mdo 8:29-31 – Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
7 Ukurasa 61 Kipengele II-C
8 Ukurasa 62 Kipengele II-C-2
Made with FlippingBook - Share PDF online