Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 4 9

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Katika maswali haya hapa chini utagundua kwamba shabaha yake kubwa ni juu ya kuwa mahiri katika taarifa na kweli zinazoambatana na hoja zilizomo katika kipengele cha kwanza cha video. Kuwa makini katika kuhakikisha kwamba majibu ya mwaswali yanawapa wanafunzi uelewa uliokusudiwa katika malengo ya somo ya sehemu ya kwanza. Hakikisha unaangalia saa hapa, huku ukiyajibu maswali yote yaliyopo hapa chini pamoja na yale yaliyoulizwa na wanafunzi wako, na angalia kama kuna wazo lolote lililo tofauti ambalo linaweza kukutoa kwenye kuzichunguza kweli muhimu na hoja kuu. Kanisa la Kikristo mara zote limepinga uzushi wa Pelagia [Pelagianism] ambao unafundisha kwamba mwanadamu wa asili ana uwezo wa kuwa na shauku ya kumtafuta Mungu na kutii amri zake. Pelagio alikuwa mtawa Mwingereza aliyekwenda Roma kufundisha theolojia takriban mwaka 380 BK. Baada ya kusoma sheria na balagha ya Kirumi na baadaye theolojia huko Uingereza na Roma, hatimaye alihamia Afrika Kaskazini ili kuepuka uvamizi wa Wagothi waliovamia Roma mnamo AD 410 ambapo mahubiri yake yalivutia idadi ya wafuasi wenye uwezo. Mafundisho yake yalipingwa vikali na Augustine, askofu wa Hippo (katika Algeria ya sasa). Uzushi wa Pelagia ulilaaniwa na makanisa kwenye Baraza la Carthage mnamo 418 na Baraza la Efeso mnamo 431. Pelagio na wafuasi wake walifundisha nini? Hakuna dhambi ya asili • Watu wote wamezaliwa huru na wasio na hatia (si waovu wala wenye hatia). • Ingawa huenda Adamu alitoa “mfano mbaya,” kila mtu anaishi akiwa na kile alichopewa na Mungu tu, wala si asili ya dhambi iliyorithiwa. • Mwanadamu ana uwezo wa asili wa kukataa uovu, kumtafuta Mungu na kutii amri za Mungu. • Kwa hiyo, neema ya Mungu ni uwezo wa asili unaotolewa na Mungu unaowawezesha wanadamu kumtafuta na kumtumikia.

 9 Ukurasa 63 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

 10 Ukurasa 65 Kipengele I-B

Made with FlippingBook - Share PDF online