Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 5 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Wokovu unagharamiwa

Neema ya Mungu inatupa: • Utashi wa asili unaotuwezesha kuchagua yaliyo mema au mabaya. • Ufunuo wake ili tuweze kuelewa yaliyo mema na mabaya. Hata hivyo, kwa sababu kila mwanadamu yuko huru kwa asili kumkubali au kumkataa Mungu na kutii au kutotii amri zake: • Wale wanaomkubali Mungu na kumtii wanapata neema ya wokovu. • Wale wanaomkataa Mungu na kutokumtii wao wanapata hukumu. Kinyume na Pelagio, mapokeo halisi ya Kanisa yanasisitiza kwamba asili yetu ya dhambi inatuzuia kufanya hatua yoyote ya hiari ya kuchagua mahusiano na Mungu au kutii amri zake. Watu wote wanaingia ulimwenguni wakiwa wamepotoka kwa sababu ya dhambi. Katika hali hiyo, hakuna mtu anayeweza kutambua kuwa anamwitaji Mungu au kuwa na shauku ya kuwa na mahusiano naye bila kwanza Mungu kuchukua hatua ya kumvuta kwake. Biblia inasema, Yohana 6:44 – Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba aliyenipeleka. Nami nitamfufua siku ya mwisho. (rej. 2 Pet. 1:3). Wakala ambaye Baba humtumia kuwavuta watu kwake ni Roho Mtakatifu. Hii ndio dhana kuu ya sehemu hii. Bila kazi ya Roho Mtakatifu hakuna mtu ambaye angeelewa kwa hakika Mungu ni nani, kutafuta kumjua huyu Mungu wa kweli, au kukiri kwa undani uhalisia wa hali yake ya dhambi na hatia yake mbele zake. Kwa hiyo, imani, wokovu, haki, na utii huja kikamilifu kwa njia ya neema ya Mungu na inaweza tu kupokelewa kama kipawa kisichopatikana kwa sifa na vigezo vya kibinadamu. Utashi wa mwanadamu hauwezi kumchagua Mungu wa kweli pasipo wito wa neema wa Baba na uwezeshaji wa neema wa Roho wake Mtakatifu. Isaya 64:6 – Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo. (rej. Zab. 143:2).

Made with FlippingBook - Share PDF online