Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 5 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Waefeso 2:8-9 – Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; [9] wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. (ling. Rum. 9:11-12, Rum. 11:6, Gal. 5:4). Tito 3:5 – ... alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu (linganisha. 1 Kor. 12:3). Wachungaji na wengine wanaohusika katika kumshauri mtu aliyetubu hawapaswi hata kidogo kudharau hisia za kweli. Huzuni ya kweli ya kimungu inapaswa, kwa kweli, kutokeza uchungu wa kihisia unaoonekana (ingawa kiasi cha kuonyeshwa kwa hisia hizo hutofautiana sana kulingana na haiba ya mtu binafsi na utamaduni husika). Hata hivyo, hofu ya matokeo na aina nyingine za “huzuni za kidunia” zinaweza pia kutoa ishara za kutokuwa sawa kihisia. Kwa hiyo ishara hizi za hisia, zenyewe peke yake, si kiashirio cha uhakika cha toba ya kweli. Kufundishika (utayari wa kukubali kusahihishwa bila kujihesabia haki au kujitetea, na hamu ya kufundishwa jinsi ya kurekebisha tabia ya zamani) ni kiashiria thabiti zaidi kwamba mtu amekuwa na badiliko la kweli la moyo. Tunashughulika na viongozi wa Kikristo wacha Mungu ambao wamethibitika na wanastahili heshima kubwa. Hata hivyo, hata Wakristo wanapambana na dhambi na viongozi wa Kikristo mara nyingi huwa na fursa chache sana ambapo wanaweza kuwa wawazi kuhusu mapambano yao. Mafundisho juu ya toba yanaweza kufungua mlango kwa wanafunzi kushirikishana kuhusu majaribu haya. Mwombe Roho Mtakatifu akufanye uwe makini kuziona fursa hizi. Ikiwa inafaa, liongoze darasa katika wakati wa maombi kwa ajili ya wokovu wa wapendwa wao na kuombea maisha ya utakatifu binafsi na ule wa kusanyiko miongoni mwa watu wa Mungu.

 11 Ukurasa 69 Kipengele II-B-2-c

 12 Ukurasa 76 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - Share PDF online