Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 5 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu Sehemu ya Kwanza
MAELEZO YA MKUFUNZI 3
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 3, Uwepo Wenye Nguvu wa Roho (Sehemu ya Kwanza). Lengo la jumla la moduli ya Mungu Roho Mtakatifu ni kuwawezesha wanafunzi wako kumuelewa Roho Mtakatifu ni nani (nafsi) na kile anachofanya (kazi), kuweza kutetea ufahamu huu kwa kutumia Maandiko, na kuona maana ya kweli hizi katika huduma ndani ya Kanisa na kupitia Kanisa. Tafadhali zingatia tena kwamba kweli hizi zimeelezewa kwa uwazi katika malengo ya somo. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na muda wako wa kukaa na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kukazia malengo haya katika kipindi chote darasani, ndivyo unavyozidi kuongeza uwezekano wa wanafunzi kuyaelewa na kuona namna yalivyo muhimu. Huu ni wakati wa ushuhuda kuhusu kazi ya Roho katika maisha ya wanafunzi. Kama kawaida, hakikisha unawasimamia na unawaongoza juu ya suala la muda. Hivyo ni muhimu kuamua ni wanafunzi wangapi uwape nafasi na watoe shuhuda zenye urefu wa muda gani. Umuhimu wa zoezi hili ni kung’amua ikiwa wanafunzi tayari wana uzoefu juu ya kazi ya Roho katika kuleta upya wa maisha. Kauli ya Mpito: Neno la kibiblia linalomaanisha kazi ya Roho ya kufanya vitu kuwa vipya ni “kuzaa upya” [ Regeneration ]. Litilie maanani neno hili tunapoendelea kuchunguza kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini. Baada ya zoezi la kushirikisha shuhuda kukamilika, hakikisha una sisitiza kwamba tofauti miongoni mwa Wakristo juu ya masuala yanayoibua mijadala na mabishano hazitakiwi kuathiri uwezo wetu wa kupendana na kusikilizana . Wakumbushe wanafunzi kwamba kwa sababu wao tayari wamejua misimamo yao kitheolojia, basi wanaweza tu kujifunza pia kutoka katika misimamo ya kitheolojia ya watu wengine. Hii (kawaida) haimaanisha kwamba watabadilisha misimamo yao, badala yake ina maana kwamba wana nafasi ya kuyasikiliza Maandiko kupitia “masikio mapya” wanapoendelea kujadiliana na wale ambao wanawakilisha mitazamo tofauti.
1 Ukurasa 81 Utangulizi wa Somo
2 Ukurasa 82 Kujenga Daraja – Sehemu ya 1.
3 Ukurasa 83 Kujenga Daraja – Sehemu ya 3.
Made with FlippingBook - Share PDF online