Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
2 5 4 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Sasa tunataka tuzungumze juu ya kile kinachotokea kwenye maisha ya mtu pale anapookoka. Neno kuokoka hapa tunamaanisha ile kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu inayotupelekea kushawishika kuitikia kwa Yesu Kristo kama Bwana. Wakati wa kuokoka: • Tunatubu dhambi zetu, • Na kwa imani tuna mpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi na kuweka imani yetu yote na tumaini kwakwe kwa ajili ya wokovu, • Ambao tunapokea kama kipawa cha bure cha neema kutoka kwa Mungu. Mathayo 18:3 -... akasema, “Amini, nawaambia msipoongoka [ strepho - kugeuka] na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (rej. Mt. 13.15; Marko 4.12). Matendo 3:19 - Tubuni basi, mrejee [ epistrepho - kugeukia uelekeo fulani]. Pale tu tunapotubu na kumgeukia Mungu kwa imani katika Yesu, Yeye anafanya mambo kadhaa ndani yetu, kwa msingi wa kazi ya Kristo lakini kupitia nguvu za Roho Mtakatifu . Mwanatheolojia wa Kiorthodoksi wa Kirusi aitwaye Sergius Bulgakov (1871 1944) anatoa tathmini nzuri sana kwamba siku ya Pentekoste, “Kushuka kwa Roho Mtakatifu katika ulimwengu, ili akae nasi milele, ndiko kushuka kwake kwa mwisho; hatatokea kupaa tena kurudi mbinguni wala hatazuiliwa na chochote” (The Comforter, trans. Boris Jakim, Grand Rapids, MI: Wm. B. Eerdmans, 2004, uk. 277). Kazi iliyoanzishwa siku ya pentekoste (na kudhihirishwa kupitia jamii mpya – Kanisa la Mungu) ni kazi ambayo inaendelea hadi vitu vyote vitakapofanywa upya. Roho Mtakatifu katika ulimwengu huu anafanyia kazi matokeo ya ushindi wa Kristo dhidi ya dhambi, mauti, na shetani uliopatikana mara moja tu na ikatosha. Kazi ya Roho katika Kanisa ni kionjo halisi cha kile ambacho Roho mwenyewe siku moja atakikamilisha katika ulimwengu wote (ingawa kurudi kwa Kristo na hukumu ya waovu ni lazima vitokee kabla ya uumbaji huu mpya).
4 Ukurasa 85 Kipengele II-B
5 Ukurasa 89 Kipengele II-C-4-d
Made with FlippingBook - Share PDF online