Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 5 5

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Profesa Myron Augsburger anasimulia hadithi ya mwinjilisti mzungu ambaye alienda na kufanya uinjilisti wa mikutano miongoni mwa watu weupe huko pande za Kusini nyakati ambapo jamii ilijawa na ubaguzi uliohalalishwa kisheria na kijamii. Alihubiri ujumbe wa kawaida tu wa Injili lakini ulipofika muda wa kuwaita ili kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi, aliwaomba watu waende mpaka mbele kabisa. Aliyesimama pale mbele alikuwa mchungaji mweusi kutoka katika moja ya makanisa ya watu weusi katika jiji hilo. Mwinjilisti aliwaambia watu kwamba mchungaji ataweka mkono wake juu ao na kuomba pamoja nao maombi ya kumwalika Yesu katika maisha yao. Kwa nini alifanya hivyo? (Alitaka waelewe kwamba wokovu unahusisha kitendo cha wao kuingia katika familia. Mtu anayetaka kukwepa Jehanamu lakini hataki kufanyika mwanafamilia huyo hauchukulii wokovu katika misingi yake). Unaweza kukubaliana au kutokubaliana na mbinu za mwinjilisti yule lakini ninaamini kwamba kila mwongofu aliyepatikana alikuwa wa kweli. Kuasiliwa ni sehemu ya kifurushi kinachokuja na wokovu. Sio kitu ambacho kila mtu hupitia au angechagua kupitia. Kuasiliwa (kufanywa wana) ni lugha nzuri sana kwa sababu ni lugha ya kifamilia. Mwanatheolojia Thomas C. Oden anapenda kuita Ubatizo na Meza ya Bwana kuwa ni “kuoga” na “mlo.” Ni kana kwamba haipingiki kwamba vitu viwili ambavyo mtu asiye na makazi anahitaji zaidi ni kuoga na mlo. Tunapofanywa wana ili kuingia katika familia ya Mungu tunapewa vitu hivyo vyote viwili katika familia yetu mpya. Tunaoshwa katika ubatizo na kulishwa katika ushirika mtakatifu. Kufanywa wana kunaakisi kiini cha kazi ya Roho katika kutufanya kuwa familia ambayo inaundwa na Mungu kama Baba yetu, Kristo kama kaka yetu mkubwa, na watu wote wa Mungu kama kaka na dada zetu. Vitabu vya marejeo tutakavyo visoma katika kozi hii vinaonyesha tofauti hizi za msingi. Theolojia ya Millard Erickson kuhusiana na ubatizo wa Roho Mtakatifu inawakilisha mrengo wa mapokeo ya Reformed/Kibaptisti wakati Craig Keener (japokuwa anahudumu katika madhehebu ya kibaptisti ya watu “weusi”) anaandika kwa uwazi na uzoefu wa mapokeo ya Kipentekoste/Karismatiki.

 6 Ukurasa 91 Kipengele III-C-2

 7 Ukurasa 92 Kipengele III-C-3

 8 Ukurasa 95 Kipengele I-A

Made with FlippingBook - Share PDF online