Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
2 5 6 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Waelekeze wanafunzi kwamba tunasoma kutoka katika mitazamo yote miwili kwa sababu kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa pande zote mbili. Kwa kweli, tuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa mwandishi (iwe Erickson au Keener) ambaye yuko nje ya mapokeo na tamaduni zetu kiimani kwa sababu tutakuwa tunasikia maarifa kutoka kwao ambayo kawaida yanaweza yasiwasilishwe kwetu katika muktadha wa kanisa tuliouzoea. Wahimize wanafunzi kumpa kila mwandishi haki ya kusikilizwa na angalau waweze kujibu hoja zao za msingi kwa kuunda na kutetea imani yao kuhusu theolojia ya ubatizo wa Roho. Msisitizo mkubwa zaidi katika Biblia, na kipengele kikuu zaidi cha mila au mapokeo yetu ya makanisa ya Matengenezo [Reformed], hupatikana katika kazi ya Roho katika kumpa mwanadamu faida zote za Mungu zinazomjia kwa njia Yesu Kristo. Imani katika Yesu Kristo ndiyo njia ambayo kwayo faida zote zinapokelewa kama vile kuhesabiwa haki, kutakaswa, na uzima wa milele, na kupitia kwa Roho Mtakatifu wokovu huu ni halisi.
9 Ukurasa 101 Kipengele III-B-3
~ “The Person and Work of the Holy Spirit with Special Reference to Baptism in the Holy Spirit.” [kutoka kwenye ripoti iliyopitishwa na Mkutano wa The General Assembly of the former Presbyterian Church, U.S. (Southern) in 1971] at http://home.regent.edu/rodmwil/tp04.html
Kazi ya Kristo haikumalizika pale alipokuwa ameupata wokovu kwa ajili ya watu wake na kupata umiliki halisi wa baraka za wokovu. Katika shauri la ukombozi alijitwika jukumu la kuwaweka watu wake wote katika umiliki wa baraka hizi na anafanya hivi kwa njia ya Roho Mtakatifu, ambaye anachukua vitu vyote vya Kristo, na kutupatia sisi.... [Imani] hutuwezesha kuchukua na kumiliki kile tunachopewa katika Kristo, na kuingia kwa kina zaidi na zaidi katika kuufurahia umoja uliobarikiwa kati yetu na Kristo, ambao ni chanzo cha utajiri wote wa kiroho.
10 Ukurasa 101 Kipengele III-B-4
~ Lewis Berkhof. Systematic Theology . Grand Rapids, MI: Eerdmans, 1941. uk. 449.
Made with FlippingBook - Share PDF online