Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 5 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Ingawa mapokeo ya Matengenezo yangeweza kuthibitisha kwamba “Ukamilifu wa Roho Mtakatifu” (kama kwa huo tunamaanisha kwamba mwamini hupokea kwa hakika Roho ambaye alitulia juu ya Kristo na kuunganishwa kikamilifu na Kristo kupitia tukio hili) unapokelewa wakati wa kuongoka na kwamba huo ndio “ubatizo katika Roho Mtakatifu,” wangetaka sana kusisitiza kwamba huwezi kumpokea “zaidi” Roho Mtakatifu zaidi ya vile unavyompokea wakati wa wokovu. Theolojia ya Matengenezo haiwezi kuuita ubatizo wa Roho “kujazwa kwa Roho Mtakatifu” kama Wapentekoste wengi wanavyofanya, lakini badala yake itahifadhi neno hilo kwa ajili ya uzoefu wa kibinafsi na Roho Mtakatifu ambao unatazamwa kama tendo la ndani ya mtu la ubatizo wa Roho: Ubatizo na Kujazwa: Kutofautishai kati ya maneno haya kuna umuhimu mkubwa kwa sababu kunahusisha mambo mengi sana. Kwa kweli maneno ‘ubatizo’ na ‘kujazwa’ mbali na kuwa ni visawe, bado yana maana zilizo kinyume. Katika ubatizo tunachovywa ndani ya kitu [kimiminika] fulani. Katika kujazwa kitu [elementi] hicho kinamiminwa ndani yetu. Ubatizo maana yake tuko ndani ya Roho. Kujazwa kunamaanisha Roho yuko ndani yetu. Ubatizo huu wa Roho, kama vile ubatizo wa maji ni wa kwanza, na kwa mujibu wa ujumbe ulio wazi wa Maandiko, [ubatizo wa Roho] haurudiwi kamwe. Kwa upande mwingine, kujazwa kunaweza kujirudia au kunaweza kusitokee kamwe. Ubatizo ni tukio la kihistoria . Kujazwa ni uzoefu wa kibinadamu . Siku ya Pentekoste, yote mawili yalifanyika kwa wakati mmoja. Kwa kweli, hilo laweza kutokea, na wakati fulani hutokea hivyo hata leo, na mwamini anaweza kujazwa na Roho baada tu kumpokea Yesu na kuokoka. Lakini ingawa ni kweli, bado hili liko mbali sana na kuwa halisi. Ama kwa kutojua ukweli au kushindwa katika kutilia maanani, ujazo wa Roho mara nyingi hutokea muda fulani baada ya uongofu.” ~ J. Oswald Sanders. The Holy Spirit and His Gifts. Revised and Enlarged Edition. Contemporary Evangelical Perspectives Series. Grand Rapids: Zondervan, 1970. uk. 65. Utimilifu wote wa Roho hupokelewa wakati wa kuongoka, lakini kuuishi utimilifu huo kunaweza kuja hatua kwa hatua.

 11 Ukurasa 102 Kipengele III-B-5

Made with FlippingBook - Share PDF online