Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 5 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Mwanatheolojia J. Rodman Williams anatupatia mfano mzuri kuhusu mtazamo huu anapoandika: Kwa neno la ziada kuhusu “ubatizo katika Roho Mtakatifu”: Maana ya usemi huu inaeleweka vyema zaidi kulingana na namna Yesu mwenyewe anavyoutumia: “Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache” (Mdo 1:5). Kama tungekuwa na maneno ya awali tu ya Yohana Mbatizaji, ubatizo katika Roho Mtakatifu ungeweza kuonekana kuwa unamaanisha kuzaliwa upya, yaani ubatizo wa Yohana katika maji ulikuwa ni maandalizi ya nje katika maji kwa ajili ya tendo la ndani la kupokea maisha mapya, au kuzaliwa upya, ambako huletwa na Yesu kwa tendo la kubatizwa kwa Roho. Vile vile Calvin katika kutoa maoni yake juu ya Mathayo 3:11, anasema, “Kristo pekee ndiye anayetoa neema yote ambayo inawakilishwa kwa njia ya mfano na ubatizo wa nje. . . na kuwapa Roho wa kuzaliwa upya.” (Commentaries, Harmony of Mathew, Mark, and Luke, 1.199 , Beveridge trans.). Hoja ni kwamba, vyovyote ambavyo Yohana Mbatizaji anaweza kuwa aliyaelewa maneno yale, hakuna maelezo yoyote yanayotolewa kuhusiana na maneno hayo katika kitabu chochote cha Injili. Kwa hivyo maneno ya Yesu katika Matendo ya Mitume ni thabiti (iwe yanatazamwa kama tafsiri ile ile au tafsiri mpya). Na kama tulivyokwisha kuona, lazima yalimaanisha hasa kile ambacho alikusudia kufanya kwa njia ya Roho kwa ajili ya kuiwezesha huduma... Kwa bahati mbaya, Calvin katika Maandiko yake anazungumza kuhusu ubatizo katika Roho kama “neema [au karama] za Roho Mtakatifu zinazoonekana wazi zinazotolewa kwa kuwekewa mikono”, na anasema, “Si jambo jipya kabisa kuashiria neema hizi kwa kutumia neno ubatizo.” (4.15.18, Battle trans.). Katika kauli hii Calvin anaenda mbali zaidi ya mtazamo unaohusianisha ubatizo wa Roho na tendo la kuzaliwa upya. Na kwa kufanya hivyo yuko karibu zaidi na picha iliyopo kitabu cha Matendo ya Mitume. ~ J. Rodman Williams. Renewal Theology: Systematic Theology from a Charismatic Perspective [Three Volumes in One], Vol. 2. Grand Rapids, MI: Zondervan, 1996. uk. 179, maelezo ya chini ya 80. Williams anaendelea kuonyesha kwamba kwa wale wanaosoma simulizi za kitabu cha Matendo ya Mitume kama ndio msingi wa fundisho, ubatizo katika Roho Mtakatifu umehusianishwa zaidi na maneno kama kumiminiwa (Mdo 2:33, 10:45), kushukia (Mdo 10:44, 8:16, 11:15), kujilia (Mdo 1:8, 19:6, rej. Yohana 1:32) na kujazwa (Mdo 2:4, 13:52) kuliko maneno kama kuongoka/kuzaliwa upya. Hili halipingi kazi ya msingi ya Roho ya kuzaa mara ya pili lakini linatofautisha

 12 Ukurasa 106 Kipengele III-C-3-b

Made with FlippingBook - Share PDF online