Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 5 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
kitendo hiki na “ubatizo wa nguvu kwa ajili ya ushuhudiaji na utume” (taz. Renewal Theology, Vol. 2, kurasa za 191-207).
Swali muhimu la kuwafanya wanafunzi kuzingatia ni, “ Je, kuna namna moja tu ya kibiblia? ” Biblia iko wazi kwamba mtu hawezi kuwa Mkristo hata kidogo pasipo kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake. Hili linasemwa kwa watu wote nyakati zote na lugha zote (Rum. 8:9). Hata hivyo, ingawa Wakristo wote wana uzoefu wa kwanza wa uhakika na Roho Mtakatifu, je, ni kweli kwamba Wakristo wote lazima wawe na uzoefu unaofana wa Roho Mtakatifu baada ya hatua hii? Kwa maneno mengine, “Je, inawezekana kwamba Biblia inafundisha mitazamo hii yote?” Je, kuna kitu chochote kibaya katika mtazamo kwamba watu katika Biblia (na watu wa leo) hawakuishuhudia kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha yao kwa njia inayofanana? Kuhusiana na uhusiano kati ya karama na tunda la Roho John Stott ameandika: “Roho huwapa Wakristo tofauti tofauti karama mbalimbali. . . bali hutenda kazi ili kuzaa tunda lile lile ndani ya wote” (ubatizo na ujazo) . Labda tunaweza kusema vile vile, kwamba mara Roho anapokaa ndani ya mtu (wakati wa kuongoka) basi huwawezesha watu kwa njia tofauti, kwa nyakati tofauti, na kwa madhihirisho tofauti, lakini wakati wote kwa kusudi moja ambalo ni kuzalisha maisha ya Kristo ndani yao.
13 Ukurasa 109 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Tafadhali chunguza ili kuwa na uhakika kwamba wanafunzi wanaelewa na wana maendeleo mazuri katika ufafanuzi (exegesis) wao wa Kitabu cha Warumi 8:1-27. Wakumbushe kuhusiana na kazi ya Huduma na ujibu maswali yoyote ambayo wanaweza kuwa nayo.
14 Ukurasa 114 Kazi
Made with FlippingBook - Share PDF online