Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 6 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu Sehemu ya Pili

MAELEZO YA MKUFUNZI 4

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 4, Uwepo Wenye Nguvu wa Roho (Sehemu ya Pili). Lengo la jumla la moduli ya Mungu Roho Mtakatifu ni kuwawezesha wanafunzi wako kumuelewa Roho Mtakatifu ni nani (nafsi) na kile anachofanya (kazi), kuweza kutetea ufahamu huu kwa kutumia Maandiko, na kuona maana ya kweli hizi katika huduma ndani ya Kanisa na kupitia Kanisa. Tafadhali zingatia tena kwamba kweli hizi zimeelezewa kwa uwazi katika malengo ya somo. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na muda wako wa kukaa na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kukazia malengo haya katika kipindi chote darasani, ndivyo unavyozidi kuongeza uwezekano wa wanafunzi kuyaelewa na kuona namna yalivyo muhimu.

 1 Ukurasa 117 Utangulizi wa Somo

Dhana ya Roho ambaye anatoa karama haijaibuka tu katika Nyaraka, badala yake, imejengwa juu ya misingi imara wa mafundisho ya Agano la Kale na Injili kuhusu Roho na ahadi ya Kimasihi.

 2 Ukurasa 120 Kipengele I-A

Msingi wa Agano la Kale: Karama za Masihi

Isaya 11:2 – Na Roho ya BWANA itakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu , roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA. Ufafanuzi huu wa maeneo saba ya uwezesho wa kiungu juu ya Mfalme wa Kimasihi unaanza na Roho wa Bwana. Hii inaashiria kwamba Roho, yeye mwenyewe, ni wa kiungu, na pia ndiye yule ambaye ‘uwepo wake’ unasababisha Bwana mwenyewe kukaa ndani ya Mfalme wake. Udhihirisho katika yale maeneo sita zaidi unaendeleza kweli hii katika jozi tatu: sifa za kiutawala za mfalme, hekima na ufahamu; uwezo wake wa kivitendo, ushauri na nguvu; na sifa zake za kiroho, ujuzi na kicho. Zote hizi ndizo sifa za mtawala wa kweli. ~ J. Alec Motyer. Isaiah. Tyndale Old Testament Commentary. Nabii anafundisha kwamba Masihi ajaye atatawala kupitia vipawa (karama) zinazotoka kwa Roho Mtakatifu na kudhihirisha uwepo wa Roho na nguvu. Watafasiri wa Kikristo mara nyingi wamezitaja hizi kama karama saba za Roho. Uelewa huu wa Agano la Kale wa njia ambayo Roho hufanya kazi ili kutimiza

Made with FlippingBook - Share PDF online