Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 6 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

mapenzi ya Mungu pia hutusaidia kufasiri lugha fulani ya ajabu katika Kitabu cha Ufunuo. Ufunuo 1:4 – Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi (Pia Ufu. 3:1, 4:5, 5:6). Katika toleo The New Living Translation, mstari huu unatafsiriwa, “ from the sevenfold Spirit before his throne ” [zitokazo kwa madhihirisho saba ya Roho]. Kutoka kwenye roho saba inamaanisha kutoka kwa Roho Mtakatifu katika utimilifu wake ulio mara saba. Wengine wameona hapa kama panaongelea viumbe vya kimalaika; lakini kwa kuwa kishazi kinachotangulia kinamaanisha Mungu Baba, na kinachofuata kinamaanisha Mungu Mwana, basi ni jambo la uhakika kwamba Yohana alijumuisha maneno hayo akimaanisha Mungu Roho Mtakatifu, na hivyo alijumuisha Nafsi zote za Mungu Mmoja. Katika maeneo mengine Agano Jipya linaongelea juu ya Roho Mtakatifu katika wingi wake wa kazi azifanyazo (rej. Ebr. 2:4; 1 Kor. 12:11; 14:32; Ufu. 22:6). ~ George Eldon Ladd. A Commentary on the Revelation of John. Kurasa za 24-25. Kwa kuwa saba ni nambari inayoashiria ukamilifu katika maandishi ya maandiko, hii pia ni njia ya kusisitiza kwamba Roho ameubeba ukamilifu wa nguvu na uwepo wa Mungu. (Tazama pia kitabu cha Ray Pritchard, “Seven Spirits of God,” Names of the Holy Spirit, Chicago: Moody Press, 1995, kurasa za 207-20.)

Muktadha wa Agano Jipya: Kipawa cha Wokovu cha Masihi

Mtazamo wa mapokeo ya Matengenezo [Reformed] kwamba kazi ya Roho inatuunganisha na Kristo uko wazi sana katika maandiko ya Paulo. Kuna muendelezo katika kazi ya Roho. Roho anakuja juu ya Masihi ili kumpa vipawa kwa ajili ya utawala wake wa kifalme. Wale wote wanaopokea wokovu basi wanawekwa “ndani ya Kristo,” na kufanyika “ukuhani wa kifalme.” Na wokovu huu unakuja tu kama “kipawa.” Ni “kipawa” cha kwanza kabisa cha Roho.

Made with FlippingBook - Share PDF online