Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 2 6 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Rum. 5:15-17 – Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. 16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. 17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Kipawa cha utoaji cha Wakorintho kilichukuliwa na Paulo kama kilichotiririka moja kwa moja kutoka katika kipawa cha neema iletayo wokovu! 2 Kor. 9:13-15 – kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote. 14 Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu. 15 Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo. Kwa hivyo wokovu wa wale wanaoamini unaonekana kama kipawa cha kwanza cha neema – kipawa ambacho ni chimbuko la vipawa vingine vyote. Neno lingine ambalo kawaida linatumika ni charism [kwa wingi charismata], limechukuliwa kutoka katika neno la Kiyunani linalotafsiriwa kama “neema” ( charis ) na maana yake halisi ni “karama za neema.” Kuna kundi la maneno yenye chimbuko lake katika shina la neno la kiyunani char.... ni muhimu kwamba furaha, kushangilia, kutoa, kushukuru, neema, na vipawa vyote vinatokana na shina hilo hilo moja. Pia ni muhimu kwamba maneno yote haya yanahusiana na furaha au kutoa shukrani. ~ Harley H. Schmitt. Many Gifts, One Lord. Kumbuka kwamba neno hili linatukumbusha kuwa karama hazitoki kwetu, kwamba ziko chini ya udhibiti kamili wa Roho na kwamba hazipaswi kuwa chanzo cha kiburi, bali cha shukrani tu.

 3 Ukurasa 120 Kipengele I-B

Made with FlippingBook - Share PDF online