Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 6 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Madhihirisho ya Roho Mtakatifu yamekusudiwa kulisaidia Kanisa la Mungu kwa namna ambayo linawezeshwa kutimiza utume wa Mungu ulimwenguni. Muktadha wa mafundisho kuhusu vipawa au karama za kiroho ni wa kijumuiya kabisa. Tabia ya Kimagharibi ya kutanguliza kujifikiria kibinafsi (Karama yangu ni ipi?; Nina karama ya imani; huduma yangu ni ipi?, n.k.) badala ya kufikiria kama mshirika katika kusanyiko itapelekea kupotosha jinsi karama za rohoni zinavyofafanuliwa na kutumika. Katika Warumi 12, Paulo anamalizia somo lake juu ya karama za rohoni kwa kutoa maelekezo haya. Warumi 12:9-13 – Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema. 10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; 11 kwa bidii, bila kulegea; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; 12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali; 13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. Muktadha mzima wa 1 Wakorintho 12-14 unatoa ukweli kwamba vipawa vya kiungo kimoja tu katika mwili havina manufaa mpaka pale vitakapo unganishwa pamoja na vya watu wengine na kutoa faida kwa mwili mzima. 1Wakorintho 12:7 – Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 1 Wakorintho 14:12 – Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, jitahidini kusudi mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa . (rej. 1 Pet. 4:11). Katika 1 Wakorintho 13, “sura ya upendo”, Paulo anaongea kwa ufasaha kwamba karama za rohoni hazina maana ikiwa hazitupelekei sisi kuwapenda na kuwatumikia watu wa Mungu. “ “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.” Hoja nzima ya Paulo katika 1 Wakorintho 14 ambayo inafuata “sura ya upendo” ni kwamba karama za rohoni zinaweza kuorodheshwa kwa umuhimu kwa msingi wa jinsi zinavyojenga mwili mzima wa Kristo moja kwa moja. Kwa hiyo anasema, nikinena kwa lugha nikiwa peke yangu ninamwomba Mungu, hili ni jambo jema. Kwa kweli, Paulo anasema, nataka ninyi nyote mnene kwa lugha (14:5) na zaidi

 4 Ukurasa 122 Kipengele I-B-4

Made with FlippingBook - Share PDF online