Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 6 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
ya hayo, nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote kule Korintho (14:18). Hili, Paulo asema, ni jambo jema kwa sababu linanitia nguvu katika kutembea kwangu na Mungu (14:4) na nikiwa na nguvu basi naweza kumtumikia Mungu na kuwatumikia ninyi. Lakini hiyo ni njia isiyo ya moja kwa moja ya karama kuchangia katika ustawi wa mwili. Ni nzuri na muhimu, lakini kuna njia za moja kwa moja za kuujenga mwili. Kwa hiyo ikiwa nanena kwa lugha kanisani na mtu akifasiri ujumbe huo kwa ajili ya kusanyiko, au nikitabiri au kuhubiri au kufundisha ili kusanyiko lote lifaidike mara moja, matumizi hayo ya karama ni muhimu zaidi kuliko kutumia karama ili kumnufaisha mtu mmoja kwa wakati mmoja. Bila shaka Paulo hasemi kwamba kuna karama yoyote ambayo si muhimu au si ya lazima, lakini anasema kwamba kwakuwa dhumuni la karama zote za rohoni ni kulifaidia kanisa la Mungu na utume wa Mungu katika ulimwengu, basi tunatakiwa kuhimiza vile vitu ambavyo tunafanya pamoja, kipaumbele cha kwanza kikiwa ni kumjua Mungu, na suala la faida binafsi liwe la pili. Tunaweza kufikiria juu ya hilo kwa njia hii. Kama baba anayeitunza familia yake, inaweza kuwa muhimu kwangu kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi na kufanya mazoezi kwa sababu nikiendelea kuwa na afya njema basi inanisaidia kufanya kazi yangu kwa faida ya familia. Lakini nisingeweza kamwe kuchagua kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi wakati familia yangu inanihitaji niwafanyie jambo lingine kwa wakati huo. Kwa maneno mengine, faida ya mtu binafsi ya kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi ilikuwa tu ili niweze kuhudumia familia yangu vizuri zaidi. Ikiwa ningeanza kutumia ukumbi wa mazoezi kama kisingizio cha kutokutimiza majukumu yangu ya kifamilia, kusingekuwa na maana ya kwenda. Hilo linaonyesha hasa kile ambacho Paulo anasema. Bila shaka unatakiwa kuiimarisha kila karama ambayo Mungu amekupa kwa kusudi la kukua katika Yeye. Lakini usipoteze shabaha. Yote haya ni kwa manufaa ya watu wote. Karama ambazo hutumikia mwili mzima moja kwa moja daima ni muhimu zaidi katika maana ya ushirika kuliko karama zinazomjenga mtu binafsi. (Tunapaswa kutambua kwamba Paulo anaandika sehemu hii yote ili kurekebisha tatizo la matumizi ya karama za rohoni. Wakorintho walikuwa wakitafuta kupata vyeo vya kiroho kwa kuonyesha kwamba walikuwa na karama fulani. Huu si muktadha usio na usuli bali ni muktadha wa kusahihisha. Bila shaka, hili linaathiri namna Paulo anavyoandika kuhusu karama kwa watu wa Korintho). Paulo anakubaliana kabisa na Petro ambaye anasema kwamba kusudi la karama za rohoni ni “ili katika kila jambo Mungu atukuzwe kupitia Yesu Kristo” (1 Pet. 4:11).
Made with FlippingBook - Share PDF online