Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
2 6 6 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
“Kitu chochote, tukio lolote, au mtu yeyote anayetumika kama chombo cha Roho, au anayemdhihirisha Roho, au anayeakisi utendaji wa Roho, huyo ni karama ya rohoni. (pneumatikon ) (Baker Encyclopedia of the Bible, Vol. 2, uk. 1993). Ninaamini katika kazi isiyo na kikomo ya ubunifu ya Roho ili kutoa uwezo wowote unaohitajika kwa ajili ya kulijenga Kanisa. Kwa hiyo, ninaamini kwamba karama zinaweza kuwepo ambazo hazikutajwa (au hazikuwepo) wakati wa Agano Jipya. Hii inaweza kuwa sababu kwa nini orodha za karama katika Agano Jipya zinatofautiana sana na kwa nini hakuna maelezo ya kina yaliyotolewa juu ya aina mahususi au maudhui ya karama hizi. Mfano mmoja halisi ambao unaweza kutumika kuunga mkono hoja hii ni kwamba sanaa na muziki wakati mwingine ilitazamwa kama “karama za kiroho” katika Agano la Kale, ambazo hazikutajwa hivyo katika Agano Jipya, na bado zinaongelewa sana kama “vipawa” katika uzoefu wa kihistoria wa Kanisa. Mtazamo wa somo letu ni kwamba haimaniishi tu kwa sababu hizo hazikutajwa basi si “karama za rohoni” au kwamba hazikuwapo na kutambuliwa katika Kanisa la Agano Jipya. Orodha za karama zilizotolewa hazikukusudiwa kuwa orodha kamili zenye aina na makundi yote ya karama zilizopo, bali ziliandikwa kwa makanisa maalum, kuelezea mada fulani mahususi kwa wakati husika. Mfano: Sanaa na Muziki kama karama za rohoni katika Agano la Kale. Kutoka 31:1-5 – BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2 Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda; 3 nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, 4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, 5 na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. 1 Samuel 16:23 – Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.
5 Ukurasa 123 Kipengele I-C-2
Mada ya kufafanua karama za Roho inapaswa kushughulikiwa kwa kiwango cha kutosha cha unyenyekevu na tahadhari. Akiandika kuhusu karama za rohoni, mwanatheolojia wa Anglikana Leon Morris anaonyesha kwamba:
6 Ukurasa 124 Kipengele I-C-3
Made with FlippingBook - Share PDF online