Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 6 7
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Licha ya maelezo ambayo wengi wanatoa kwa kujiamini, bado ni vigumu kugundua kwa hakika zilikuwa nini hasa. . . . Kwa kuzingatia ugumu huo, ni jambo lisiloeleweka na la kushangaza kidogo kwamba wengine hutafsiri vipawa vyao kwa ujasiri sana. Siyo vibaya kusema kwamba hakuna karama hata moja inayoweza kutambuliwa kwa ujasiri kamili. ~ New Testament Theology. uk. 78. Jambo la maana si kwamba tunapaswa kuinua mikono yetu juu kwa kufadhaika bali kwamba tunahitaji kuwa waangalifu kuhusu imani ya kweli. Elewa kwamba karama zinatolewa ili kulisaidia Kanisa katika utume wake na kwamba uwezo unaohitajika katika kulitayarisha Kanisa kwa ajili ya utume huo unaweza kubadilika kutoka utamaduni hadi utamaduni na kutoka mahali hadi mahali. Ufafanuzi mwingi sana unaweza kuondoa uhuru wa Mungu Roho Mtakatifu kutembea ili kukidhi mahitaji ya mwanadamu yanayobadilika. Kusudi la Mungu na ujumbe wake havibadiliki lakini mbinu zake (pamoja na uwezeshaji wake) huvibadilisha kwa neema na kwa uhuru kulingana na mazingira ya mwanadamu. Katika Maandiko ya Agano Jipya na historia ndefu ya Kanisa, kuna mifano mingi ya watu walioamini kwamba kwa sababu walikuwa na karama ya uongozi, au karama ya neno, au karama ya nguvu, walikuwa wa kiroho zaidi kuliko mtu mwingine ambaye hakuwa na karama hizo. Mtume Paulo anasema kwamba hili si kweli hata kidogo. Katika 1 Wakorintho 12 na 13, anaishughulikia moja kwa moja dhana hii potofu. Kwa wengi katika Korintho, “udhihirisho wa Roho kupitia karama ya kunena kwa lugha, ulikuwa ni ushahidi wa uhakika kwamba wao ni pneumatikos (yaani mtu wa Roho, na hivyo wa ‘kiroho’)” (Gordon Fee, The First Epistle to the Corinthians, The New International Commentary on the New Testament, Gen. Ed. F. F. Bruce, Grand Rapids: Eerdmans, 1987, uk. 666.). Kutokana na mtazamo huu Paulo anatoa hoja ifuatayo: Kwanza, anasisitiza kwamba Wakristo wote wamebatizwa katika mwili mmoja, katika Roho mmoja na wote walinyweshwa Roho mmoja (1 Kor. 12:13). Kisha anahakikisha kwamba wanaelewa kwamba kuwa na karama mbalimbali za rohoni ni sehemu ya kawaida, yenye afya ya utofauti unaopatikana katika mwili wa Kristo (1 Kor. 12:14-31) na hivyo basi tofauti hizi haziwezi kutumika kukuza hali ya kiroho ya baadhi ya waamini kuwa juu ya wengine (1 Kor. 12:21-25). Hatimaye,
7 Ukurasa 128 Kipengele I-D-3
Made with FlippingBook - Share PDF online