Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

2 7 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

na sheria na hukumu za Mungu. . . . Kitendo cha kupewa Roho ilikuwa ishara ya zama za Kimasihi (taz. Isa. 42:1; 44:3; 59:21; Yoeli 2:28 na kuendelea.), na Ezekieli alifahamu jambo hili na alilitaja katika matukio ya baadaye (37:14; 39:29). Hivyo, Kwake yeye urejesho wa Israeli ulikuwa ni mwanzo wa siku za mwisho, zama za Masihi. ~ Ezekiel. The Tyndale Old Testament Commentaries. Leicester, England/Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1969. uk. 232. Roho Mtakatifu ndiye ambaye Mungu humtumia kuufanya ushindi dhidi ya uovu, uliopatikana mara moja kwa kifo na ufufuo wa Kristo, uwe halisi katika maisha ya watu wake. Kazi yako kama Mkufunzi na unayehusika na kutoa maksi na kupanga madaraja inaanza kwa uzito mkubwa zaidi sasa. Hakikisha kwamba umekusanya mapendekezo ya wanafunzi kuhusiana na Kazi za Huduma, Kazi za Ufafanuzi wa Maandiko na taarifa nyingine muhimu, kwa sababu hili litakuwa muhimu kwako katika kutoa matokeo ya jumla ya mwanafunzi. Kwa mara nyingine, busara zako kuhusiana na wanafunzi wanaochelewesha kazi zao inaweza kuamua ikiwa utakata maksi za wahusika, jambo ambalo litaathiri madaraja yao ya ufaulu baadaye, au ikiwa utawawekea maoni ya “Isiyokamilika” mpaka watakapo kamilisha kazi na kukabidhi. Vyovyote utakavyoamua kufanya kuhusiana na kazi zao, kumbuka kwamba kozi zetu kimsingi hazilengi maksi ambazo wanafunzi wanapata, badala yake tunazingatia zaidi lishe ya kiroho na mafunzo ambayo kozi hizi zinatoa. Hata hivyo, kumbuka kwamba kuwasaidia wanafunzi wetu kujitahidi kupata matokeo bora ni sehemu muhimu ya mafunzo yetu.

 12 Ukurasa 149 Kazi

Made with FlippingBook - Share PDF online