Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 2 6 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
kufanana na Kristo kunaonekana katika ukweli kwamba mitazamo na maadili yetu ya ndani yafanana na yake. [Hizi si njia mbili tofauti za kumfuata Kristo bali ni pande mbili za sarafu moja. Hakuna mtu anayeweza kudai kuwa na tabia na mitazamo ya Kristo ambaye hafuati mafundisho na kielelezo chake (Yohana 14:23; Luka 9:23-24). Vivyo hivyo, mtu ambaye kwa nje anaendana na mafundisho lakini kwa ndani hachochewi na mitazamo na maadili ya Kristo mwenyewe ni kama “shaba iliayo na upatu uvumao” ambao si kitu (1 Kor. 13)]. “Tunda la Roho” ni neno ambalo Paulo anatumia kuhusiana na tabia hizi za ndani za kufanana na Kristo. Ni kinyume kabisa cha shauku na tamaa za “mwili”. Hivyo, kama vile Mwandishi R. E. O. White asemavyo: Utakaso kimsingi si jambo hasi katika Agano Jipya, “kujiweka bila doa,” sio hasa nidhamu ya kibinafsi. Lakini ni kumiminika kwa nje kwa maisha yanayofurika ndani ya nafsi, “tunda” la Roho katika kila namna ya neema za Kikristo (Gal. 5:22-23), zinazojumlishwa kama “utakaso” (Rum. 6:22). Kuhesabiwa haki – hali ya upendeleo ya kukubalika – kunapatikana kwa njia ya msalaba; utakaso – mchakato unaoendelea wa kufanana na Kristo – unawezeshwa na Roho. Agano la Kale linaiona kazi ya Masihi kama mtu anayeingiza enzi mpya ya Roho ambayo kwayo watu wa Mungu wanawezeshwa kwa ajili ya kuishi maisha ya utakatifu. Ezekieli anaelezea enzi ya Kimasihi kwa namna ifuatayo: Ezekieli 36:26-27 – Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Akitoa maoni yake kuhusu andiko hili, John B. Taylor anasema: Matokeo ya upandikizaji huu wa kisaikolojia yatakuwa kwamba Israeli itapata “badiliko la moyo” la kweli na watakuwa, kwa mpango wa neema wa Mungu, aina ya watu ambao hapo awali walikuwa wameshindwa kabisa kuwa. Kupandikizwa kwa Roho wa Mungu ndani yao kutabadilisha nia yao na kuwawezesha kuishi kulingana ~ “Sanctification.” Evangelical Dictionary of Theology. Walter A. Elwell, ed. Grand Rapids: Baker, 1984. uk. 970.
11 Ukurasa 138 Kipengele I-C-1-b
Made with FlippingBook - Share PDF online