Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
4 0 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(1) Mungu anapomtuma Yesu duniani yeye pia anaingia ndani ya maji, si ya gharika, bali ya mto Yordani katika ubatizo, Luka 3:22. (2) Tukio hilo ni muhimu sana kiasi kwamba limeandikwa katika vitabu vyote vinne vya Injili. Kuonekana kwa Roho Mtakatifu kama hua kunawakumbusha wasikilizaji wa Kiyahudi wanaomwona Yesu akibatizwa kwamba, kama Nuhu, mtu huyu ni mpendwa wa Mungu na njia ya tumaini jipya na uumbaji mpya.
Ibid. uk. 79.
1
3. Majina na vyeo vya Roho Mtakatifu katika Biblia vinamfunua yeye kama Mpaji wa Uzima.
a. Anaitwa Roho wa Kweli (Yoh. 14:16-17; 15:26; 16:13). Yeye ndiye anayetufundisha maneno ya uzima.
b. AnaitwaRohowaUtakatifu (Rum. 1:4). Yeye ndiye anayetuwezesha kushinda dhambi na kifo.
c. Anaitwa Roho wa Neema (Ebr. 10:29). Yeye ndiye anayeleta bure maisha mapya kwa wale ambao wasingeweza kuyapata kupitia juhudi zao wenyewe.
d. Anaitwa “Roho wa Uzima” (Rum. 8:2). Ana huduma ya kuleta uzima na ndiye chanzo cha ufufuo.
Ibid. uk. 105, 123, 127, 131, 191.
C. “Palipo na Uzima kuna tumaini”: matokeo ya huduma ya uzima afanyayo Roho. Warumi 15:13 – Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Made with FlippingBook - Share PDF online