Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

5 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

hayo ni yapi? Je, tunaweza kumjua Mungu kupitia sayansi, falsafa, au sanaa? Ikiwa jibu ni ndiyo, kwa nini? Ikiwa ni hapana, kwa nini?) Karl Barth anasema: “Jaribio linafanywa [na Kanisa] kuzungumza juu ya Mungu kwa nia ya kwamba wengine wasikie kumhusu. Jaribio na nia hii kimsingi haviwezekani. Mungu si wa ulimwengu. Kwa hivyo, yeye si sehemu ya vitu ambavyo tunaweza kuviainisha na kuvielezea kwa maneno... .” (Church Dogmatics, Vol. I.2, The Doctrine of the Word of God ). Je, andiko la 1 Wakorintho 2:13 linasema nini kuhusu tatizo hili? Nini kazi ya Roho Mtakatifu katika suala zima la kumjua Mungu? Je, tunaweza kumjua Mungu kwa njia nyingine tofauti na kazi maalum ya ufunuo ya Roho Mtakatifu? Ikiwa jibu ni ndiyo, kwa nini? Ikiwa ni hapana, kwa nini? Neema ya Ajabu, Iliyoniokoa Mnyonge Mimi – Kusikia hayo kwa pendeza kama nini! Katika sehemu ya pili ya somo hili, tutajadili kazi ya Roho Mtakatifu katika kuwashuhudia watu kwa habari ya dhambi zao na kuwavuta katika imani na toba. Hili lilitokeaje katika maisha yako mwenyewe? Ni nini kilikushawishi kuwa kweli ulikuwa na hatia mbele za Mungu? Je! Roho Mtakatifu alikushawishi vipi kukiri dhambi zako na nini kilitokea baada ya muda huo wa kuungama? Wakristo wa madhehebu yote wanakiri kwamba kazi muhimu zaidi ya Kinabii ya Roho ni uvuvio wa Maandiko. Maandiko ndiyo chanzo na fimbo ya kupimia ya maarifa yote yenye mamlaka kuhusu Mungu na mapenzi yake. Hata hivyo, leo, Wakristo wanapozungumza kuhusu kazi ya kinabii ya Roho, madhehebu tofauti ya Kikristo hutofautiana katika msisitizo wao. Wengine hulinganisha huduma ya kinabii na kuhubiri (kipawa cha Roho cha kuangazia andiko fulani la kinabii), wakati wengine wanaona kazi endelevu ya maneno ya kinabii ambayo huongoza na kulielekeza Kanisa (ndani ya mipaka ya Maandiko). Ni ipi kati ya njia hizi mbili inayoelezea kwa karibu zaidi kinachofanyika katika kanisa lako mwenyewe? Roho wa Unabii

2

2

ukurasa 247  4

3

Made with FlippingBook - Share PDF online