Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 5 5

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu Sehemu ya 1: Roho Aliyenena Kupitia Manabii

YALIYOMO

Mch. Terry G. Cornett

Tunaweza kumjua Mungu Aliye hai kwa sababu tu amechagua kujifunua kwetu. Roho wa Mungu ndiye anayeweka maarifa ya Mungu katika maneno ya wanadamu na kuyafanya yajulikane kwa manabii. Roho wa Mungu ndiye aliyetupatia Maandiko na anayetuwezesha kuyaelewa na kuamini kweli ambazo Maandiko hayo yanafundisha. Pasipo kazi ya Roho, hakuna mtu ambaye angetaka kumtafuta Mungu wala hakuna ambaye angeweza kugundua jinsi alivyo. Kusudi letu katika sehemu hii, Roho Aliyenena Kupitia Manabii, ni kukuwezesha wewe kufanya yafuatayo: • Kuelezea dhana ya kibiblia ya unabii. • Kuelewa kwamba Maandiko yote ni Neno la “kinabii” kutoka kwa Roho wa Mungu. • Kuona kwamba unabii wote unahusisha “kutangaza” ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili ya mambo ya nyakati za sasa (forthtelling) , ilhali baadhi ya unabii pia unahusisha “kutabiri” tukio la wakati ujao katika mpango wa Mungu. • Kuonyesha kutoka katika Maandiko kwamba unabii ni huduma [karama] inayotolewa kwa wanawake na wanaume. • Kuthibitisha kutoka katika Maandiko kwamba unabii huja kupitia huduma ya Roho Mtakatifu. • Kuthibitisha madai ya kibiblia kwamba Roho Mtakatifu ndiye mwandishi wa Maandiko. • Kufafanua mafundisho ya uvuvio na kuangaziwa (kutiwa nuru ) na uhusiano kati ya dhana hizo. Katika sehemu hii ya kwanza tutachunguza fundisho la Biblia la uvuvio wa kinabii. Imani ya Nikea inatukumbusha kwamba fundisho hili linahusiana moja kwa moja na huduma ya Roho Mtakatifu linaposema kwamba Roho ndiye “aliyenena kwa kinywa cha manabii”.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

2

Made with FlippingBook - Share PDF online