Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 5 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(5) Mabinti wanne wa Filipo Mwinjilisti, Matendo ya Mitume 21:9
Vilevile tunaona mifano ya wanawake miongoni mwa manabii wa uongo wa Israel (Neh. 6:14; Eze. 13:17). Jinsia sio kikwazo kwa huduma ya kinabii wala si kigezo cha huduma hiyo!
b. Maandiko yenyewe yanazungumzia kumiminwa kwa Roho Mtakatifu na huduma ya kinabii ambayo ingewahusu watu waume kwa wake pasipo ubaguzi wala vikwazo. (1) Utabiri wa Yoeli (Yoeli 2:28-29) (2) Kutimia kwa unabii siku ya Pentekoste. c. Matendo ya Mitume 2:17-18 – Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenuwataota ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.
2
II. Roho Mtakatifu ndiye Chanzo cha Ujumbe wa Kinabii.
A. Unabii unahusishwa kwa karibu na kitendo cha Roho wa Mungu kuja juu ya mtu.
1. Agano la Kale
a. Wazee sabini wa Israeli, Hes. 11:25
b. Nabii Ezekieli, Eze. 11:5
c. Nabii Mika, Mika 3:8
d. Idadi kubwa ya manabii ambao Mungu aliwatuma kwa watu wake, Zek. 7:12.
Made with FlippingBook - Share PDF online