Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 6 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

d. [Mtume Paulo] anaomba, “Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo” (Efe. 1:17).... Daudi alikuwa na sheria, akifahamu hekima yote inayoweza kutamanika iliyokuwa ndani yake, na bado hakuridhika na hili, anaomba, “Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zab. 119:18)... kwa sababu chochote kisichoangaziwa na Roho wake ni giza totoro... Tukikiri kwamba tunachomwomba Mungu hakipo kwetu... hakuna mtu anayeweza kusita kukiri kwamba anaweza kuzielewa siri za Mungu, kwa kadiri tu anavyoangaziwa na neema yake (John Calvin, Institutes, II.2.21).

Hitimisho

» Unabii ni njia ya kujua kweli inayokuja kwa ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu.

2

» Nabii ni yule anayeongea kwa niaba ya Mungu kwa wanadamu.

» Unabii wote unahusisha “kuwasilisha” ujumbe wa kimungu . Wakati fulani ujumbe huu wa kimungu unahusisha “utabiri” wa matukio yajayo.

» Manabii wanaweza kuwa wanawake hali kadhalika wanaume.

» Unabii wote wa kweli unatolewa kupitia huduma ya Roho Mtakatifu.

» Roho Mtakatifu aliyavuvia Maandiko. Uvuvio ni kazi ya Roho Mtakatifu ambayo inafunua ujumbe wa kimungu na kufanya kweli ya Mungu iweze kufunuliwa kwa usahihi kupitia maneno ya kibinadamu. » Kuangazia ni kazi ya Roho Mtakatifu inayowawezesha wasomaji wa Maandiko kuelewa maana yake kwa ajili ya maisha yao na nyakati zao. Ufunuo wa Mungu unaweza tu kueleweka na kuaminiwa kupitia kazi ya Roho Mtakatifu ya kuangazia au kutia nuru.

Tafadhali chukua muda wa kutosha uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yametokana na video. Yesu alisema, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’” (Mt 4:4). Wale wanaowaongoza watu wa Mungu lazima waamini kabisa kwamba Maandiko ndiyo msingi na kipimo kwa kila jambo tunalojua kuhusu Mungu na mapenzi yake. Vile vile, viongozi wa Kikristo lazima wajue namna ya kusikia sauti ya Roho

Sehemu ya 1

Maswali kwa wanafunzi na majibu

ukurasa 249  9

Made with FlippingBook - Share PDF online