Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 7 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

(4) Kabla ya mwitikio wa mtu kwa njia ya toba na imani, lazima kwanza apokee nuru ya Roho Mtakatifu. (a) M tu wa tabia ya asili hawezi “kuyapokea mambo ya Mungu” bila msaada wa Roho Mtakatifu, Yohana 15:26; 1 Kor. 2:14. (b) K atika nyaraka zake zote, Paulo anaonyesha wazi kwamba anapolitangaza Neno la Mungu kwa watu, hazungumzi na watu wasio mtazamo wowote, hapana. Dhambi imeathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa wanadamu kuona na kukubali ukweli. Kama asemavyo Paulo, wana utaji (pazia) kwenye mioyo yao ( 2 Kor. 3:14-15 ), wamepofushwa na mungu wa ulimwengu huu ( 2 Kor. 4:4 ), wana masikio ambayo hayasikii ( Rum. 11:8 ), wanashikiliwa katika utumwa wa dhambi (Rum. 3:9, Rum. 6:17; Efe. 5:8), na ni mateka wa nguvu za kiroho zinazotawala ufalme wa giza (Efe. 6:12, Kol. 1:13). Kwa mujibu wa Paulo, ni upumbavu kuamini kwamba kwa sababu tu kweli imesemwa, watu wataweza kuisikia, kuielewa, na kuiamini. Toba inaweza kutokea tu kupitia kazi ya Roho Mtakatifu. (c)  Hakuna anayeweza kusema kwa kweli “Yesu ni Bwana” pasipo kazi ya Roho Mtakatifu, 1 Kor. 12:3. (d)  Toba ni kipawa cha neema, si matokeo ya juhudi za kibinadamu.

Mwanatheolojia wa karne ya pili Clement

wa Aleksandria alielezea kazi ya

Roho Mtakatifu kama sumaku inayowavuta wanadamu kuelekea kwa Mungu.

2

[[Toba] kwa maana halisi ni muujiza wa kimaadili, zawadi ya neema. ~ Roy Kearsley. New Dictionary of Theology . uk. 581.

Neno moja zaidi kuhusu toba: ni kipawa kutoka kwa Mungu.... Toba, ipasavyo sio kufanya matendo ya malipizi (kitubio) ambayo kwayo tunaweza kutumaini kupokea uhusiano na Mungu. Tunaweza kushukuru milele kwamba sivyo hivyo, kwa kuwa hatungeweza kamwe kuwa na uhakika kwamba tumefanya vya kutosha. Toba, badala yake, inatokana na tendo la Mungu la neema katika Yesu Kristo, ambapo macho yetu yanatiwa nuru, mioyo yetu inahakikishwa, na nia zetu kuwezeshwa kugeuka kutoka katika dhambi na utumwa kuelekea katika uzima na uhuru wa milele. Shukrani kwa Mungu! ~ J. Rodman Williams. Renewal Theology , Vol. 2. uk. 49.

Made with FlippingBook - Share PDF online