Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
7 0 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(b) T oba ni tendo linalotokea kwa sababu tumeamini kwamba yale ambayo Mungu anasema juu yetu na kuhusu hali zetu ni kweli. Kuamini yale ambayo Mungu anasema hutufanya “tubadili nia zetu” na “kugeuka”. Kwa hiyo mabadiliko ya tabia yanayotokana na toba kimantiki ni “matunda ya toba” badala ya toba yenyewe. (2) Imani ya kweli daima huzaa matendo mema. (a) Yakobo 2:17 (b) K una uhusiano wa kina kati ya imani inayozaa toba na badiliko la maisha linalotokana na imani hii. Kuzungumza juuya tobabilapiakuzungumza juuyamaishayaliyobadilika ni kama kujaribu kuzungumza juu ya moto bila moshi au joto. Ingawa moshi na joto ni matokeo ya moto, na sio moto wenyewe, bado ni njia ya uhakika ya kujua kuwa kuna kitu kinawaka. Vivyo hivyo, kuona “matunda ya toba” ndiyo njia ya uhakika ya kujua kwamba badiliko la kweli la nia kwa habari ya dhambi limetokea.
Basi, toba ni matokeo ya imani. Kwa maana mtu asipoamini kwamba kile alichokuwa amezoea kufanya ni dhambi, hatakiacha. Na ni lazima aamini kwamba adhabu inamjia mkosaji.... Vinginevyo, hatajirekebisha. ~ Clement of Alexandria (Kama mwaka. 195 B.K) Kutoka mwanzo hadi mwisho habari njema ya Injili ni kwamba toba na badiliko la maisha havitokei kwa juhudi za kibinadamu. Kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi. Kadhalika ni wakati tukiwa vipofu kiroho kutokana na hali yetu ya dhambi ambapo Roho Mtakatifu huja kwetu kwa neema ili kutuhakikisha kwa habari ya dhambi na kutupa kipawa cha toba ya kweli na imani.
2
d. Mtu aliyepokea badiliko la utashi ana nia ya kweli ya kurekebisha uharibifu uliosababishwa na dhambi alizozitenda, Luka 19:5-9.
e. Badiliko la msingi la utashi linalotokea wakati wa toba ya kweli, halitimizwi na uamuzi wa mwanadamu, bali ni matokeo ya moja kwa moja ya utendaji wa Roho Mtakatifu. (1) Uwepo wa Roho wa Mungu huidumisha roho ya mwanadamu katika utii, Zab. 51:11-12. (2) Roho humwezesha mtu kufisha matendo maovu ya mwili, Rum. 8:13. (3) Roho Mtakatifu ndani ya mtu humwezesha kumtii Mungu, Eze. 36:27.
Made with FlippingBook - Share PDF online