Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
7 4 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
³ Toba ni tendo la imani linalozalishwa na huduma ya Roho Mtakatifu. Toba inahusisha badiliko halisi la nia, moyo, na utashi na kugeuka kutoka katika njia ya maisha ya zamani. Tunda la toba ni maisha yaliyobadilika, ambayo yametolewa wakfu kwa Mungu.
Sasa ni wakati wako wa kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu mambo ambayo tumejifunza katika somo hili la Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu. Je, una maswali gani mahususi kuhusiana na yale ambayo umejifunza hivi punde? Labda baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Kuna uhusiano gani kati ya akili ya mwanadamu na uzoefu wa mwanadamu na ujuzi wa Mungu unaokuja kupitia ufunuo uliovuviwa? * Je, karama ya unabii inatenda kazi kwa wakristo leo? Je, Roho Mtakatifu anatendaje kazi kama sauti iliyo hai katika Kanisa? Je, tunatathminije kama neno la maongozi ya kinabii ni la kweli? * Kiongozi mkristo anawezaje kumsaidia mtu kutambua tofauti kati ya “huzuni ya kimungu” na “huzuni ya kidunia”? * Msingi wa Uinjilisti wa Kibiblia ni wito wa “kutubu na kuamini habari njema” za Yesu. Je, amri ya Mungu kwamba “watu wote kila mahali watubu” (Mdo. 17:30) imeelezewa na kufafanuliwa vya kutosha katika mbinu zetu za uinjilisti na mafunzo ya uanafunzi?
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
2
MIFANO
Mpenda Mazingira ya Asili
Hivi karibuni ulimwalika Devon, rafiki wa kazini kwako, kuhudhuria ibada pamoja nawe kanisani. Akasema, “Mimi kwa kweli si aina ya watu waendao kanisani. Ninaamini kwamba tunamwona Mungu vizuri zaidi tunapokuwa nje katika uumbaji wake. Jumapili nyingi asubuhi mimi hutembea tu kwenye bustani. Nafikiri ninamjua Mungu vizuri zaidi kwa kutazama mazingira ya asili kuliko watu wengi wanavyomjua kwa kusikia mahubiri.” Unamjibuje Devon?
1
Kuuza Sabuni na Kumuuza Yesu.
Watu wengi katika zama hizi wamezoea sana matangazo ya biashara. Tunasikia au kuona mamia ya matangazo ya biashara kila siku. Hivi majuzi mchungaji wako alikuomba uwe msimamizi wa kampeni ya uinjilisti yenye lengo la kuhakikisha
2
Made with FlippingBook - Share PDF online