Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 7 5

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

kila mtu anayeishi katika eneo la mitaa kumi karibu na kanisa lako anasikia habari za Yesu. Unapoanza kuweka mipango ya kuwafikia watu, unaanza kutafakari juu ya ukweli kwamba ni Roho Mtakatifu pekee anayeweza kumshawishi mtu kwa habari ya dhambi zake, na ni Roho Mtakatifu pekee anayeweza kutoa neema ya toba na imani katika Kristo. Unajua ni sahihi kufikisha “habari njema” za Yesu kwa kila mtu, lakini hutaki juhudi zako za kuwafikia ziwe kana kwamba uinjilisti ni aina ya “kiroho” ya utangazaji wa kibiashara. Ni kanuni gani zitakazokuongoza unapoweka mikakati ya kuwafikia? Je, utachukuliaje kwa uzito ukweli huu kwamba ni Roho Mtakatifu pekee anayeweza kuwavuta watu kwa Kristo? Je, kuna baadhi ya mambo unapaswa kufanya katika harakati za uinjilisti? Na je, ni mambo gani unadhani hupaswi kufanya? Wewe ni mchungaji wa kanisa. Mmoja wa washirika wako, Rhonda, anakuja kwako huku akilia. Hivi majuzi aligundua kuwa mumewe, Willie, amekuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yake. Hili limetokea kwa mara ya tatu sasa katika ndoa yao ya miaka tisa. Rhonda anakueleza, “Mchungaji, anasema anaomba msamaha lakini sina uhakika hilo linamaanisha nini. Nadhani anachojutia sana ni kwamba amekamatwa na si vinginevyo. Naomba uzungumze naye na kuniambia unachofikiria.” Unapokutana na Willie, anakuonyesha ukarimu na adabu. Anakiri kwamba alifanya kosa hilo lakini anasema, “Nilimwomba msamaha lakini siwezi kubadili nilichokifanya. Anadai kuwa ni Mkristo, kwa hiyo ikiwa hawezi kukubali msamaha wangu, basi tatizo ni lake zaidi kuliko langu.” Utamwelezaje Willie toba ya kweli ni nini na utatathmini vipi jibu lake kwa mahusia hayo? Roho Mtakatifu ndiye “aliyenena kupitia manabii.” Wakristo wanategemea Neno la kinabii (Maandiko) lililotolewa na Roho Mtakatifu ili kuwafunulia ukweli kuhusu Mungu. Kando na uvuvio na kuangazia kwa Roho Mtakatifu, kusingekuwa na njia ya kujua kwa hakika jinsi Mungu alivyo, kuelewa mapenzi yake, au kuitikia amri zake. Ni jukumu la Roho Mtakatifu kumfunua Baba na Mwana kwetu na kutuvuta katika upatanisho na Mungu. Msamaha Umekubaliwa?

2

3

Marejeo ya Tasnifu ya Somo

Made with FlippingBook - Share PDF online