Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

7 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Ikiwa utapenda kupata ufahamu wa kina zaidi kuhusu baadhi ya maarifa yaliyomo katika somo hili la Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu, basi unaweza kujaribu vitabu hivi: Thomas C. Oden. Chapter 3, “The Way of Repentance.” Life in the Spirit. Systematic Theology: Vol. Three. San Francisco: HarperSanFrancisco, 1992. Robert L. Saucy. The Bible: Breathed from God. The Victor Know and Believe Series. Bruce L. Shelly, ed. Wheaton, IL: Victor Books, 1978. Mtume Yakobo anatusihi tusisikilize tu Neno, bali tulitii. Anasema kwamba tunabarikiwa, si tunapoisikia kweli, bali tunapoitendea kazi (Yakobo 1:22-25). Sasa ni wakati wa kutafakari juu ya matokeo ya mafundisho haya katika huduma halisi ambayoMungu amekuitia. Je, mafundisho kuhusu uvuvio ( inspiration ) na kuangaziwa (kutiwa nuru, illumination ) yanahusiana vipi na kazi ambazo Mungu amekupa? Ni nani unadhani anahitaji kufahamu juu ya kweli ulizojifunza kuhusu kuhakikishwa na kutubu? Ni picha gani hasa inakuja akilini mwako unapofikiria kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu katika kuwavuta watu kwa Mungu na katika kweli yake? Mwombe Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa, si tu kweli kuu za somo hili, bali pia namna ambavyo anataka kweli hizi zitumike katika maisha na huduma yako. Omba kwa malengo mahususi. Muulize Roho Mtakatifu kama kuna namna anataka utendee kazi somo hili wiki hii hii na kisha uwe makini kuona fursa ambazo atakuletea ndani ya siku hizi. Tunamtumikia Mungu aliye hai na Roho wake Mtakatifu atatukumbusha yale ambayo tumejifunza kwa wakati muafaka tunapoyahitaji. Pengine kila mtu humu darasani tayari anaomba kwa ajili ya mtu anayemjua ambaye anahitaji kutubu na kuamini Injili. Inawezekana kwamba wewe mwenyewe uko katika mapambano na “dhambi ambayo inakuzinga kwa wepesi” (Ebr. 12:1). Ni muhimu sana tujikumbushe kwamba huduma ya neema ya Roho Mtakatifu ipo ili kukabiliana na hali kama hizi. Mungu alifanya kazi (na anafanya kazi) kwa ajili ya watu “wakati wangali wenye dhambi” (Rum. 5:8). Tafuta rafiki ambaye anaweza kuomba nawe ili Mungu awape toba wapendwa wako wasiomjua Yesu. Omba kwamba Roho akuhakikishe wewe, na wale unaowajali, kuhusu tendo lolote la dhambi lisilompendeza Mungu na kwamba aweze kumpa kila anayehusika neema ya kufikia toba ya kweli na badiliko la maisha. Tunamtumikia Mungu mwenye neema ambaye yuko tayari kutoa rehema na msaada kuliko tunavyoomba. Roho hukaa ndani ya kila mmoja wetu tulio wa Kristo. Hebu tumwombe afanye ndani yetu “kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu” (Efe. 3:20).

Nyenzo na Bibliografia.

Kuhusianisha somo na huduma.

2

Ushauri na Maombi.

ukurasa 251  12

Made with FlippingBook - Share PDF online