Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 8 1
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu Sehemu ya Kwanza
S O M O L A 3
ukurasa 253 1
Karibu katika Jina imara la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, kufanya majadiliano, na kuweka katika vitendo maarifa yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kutumia neno la kiakrostiki* la kiingereza “RABBIS” kukumbuka kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya waamini. • Kueleza maana na umuhimu wa kitheolojia wa jukumu la Roho katika kuzaliwa upya, kufanywa wana, na ubatizo wa waamini katika Kristo. • Kuelewa makubaliano na utofauti miongoni mwa wakristo kuhusiana na maana ya “ubatizo katika Roho Mtakatifu.” • Kutumia Maandiko ili kuonyesha kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ndiyo njia ambayo Mungu huwazaa upya, huwafanya wana na kuwabatiza wale wanaoweka imani yao katika Kristo Yesu. Soma Mathayo 3:1-12. Wakristo wanamheshimu sana Yohana Mbatizaji kwa vile yeye ndiye mtangulizi wa Yesu, na nabii wa mwisho na mkuu zaidi wa Agano la Kale. Lakini tunaona kwamba Yohana Mbatizaji alipohubiri, alizungumza kuhusu Yesu Mbatizaji. Yohana alifundisha kwamba ubatizo wake yeye ulikuwa wa toba (yaani, ungewasaidia watu kuonyesha kwamba walikuwa na majuto kwa ajili ya dhambi zao na kwamba walitamani kupata badiliko), lakini ubatizo ambao Yesu aliuleta ungekuwa “wenye nguvu zaidi” kuliko huu. Ubatizo huo haungekuwa wa maji tu bali na uwepo wa Roho Mtakatifu wa Mungu. Kama moto uteketezao makapi, Roho Mtakatifu angeleta si tu huzuni kwa sababu ya dhambi bali pia angeiharibu dhambi. Angalia kwa makini ishara ambayo Yesu aliichagua ili kuelezea ubatizo huu. Alisema huo utakuwa ubatizo wa moto. Maji husafisha tu uso wa kitu, moto hupenya maeneo yote na kutakasa kwa utakaso wa kudumu. Kwa maneno mengine, Yesu anatubatiza katika Roho Mtakatifu kama njia ya kutufanya wapya kabisa. Mahubiri ya Yohana Mbatizaji yanatukumbusha kwamba, tangu mwanzo Yesu alikuja, si kufa kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kutuwezesha sisi kumpokea Roho Mtakatifu. Basi na tuseme asante kwa Mungu, kwamba hakututumia Yohana Mbatizaji peke yake, bali pia Yesu Mbatizaji, ili tupate kipawa cha thamani na chenye nguvu cha Roho wake Mtakatifu anayetakasa. Yesu Mbatizaji.
Malengo ya Somo
* Akrostiki ni neno linaloundwa na herufi za mwanzo za maneno au vishazi vingine na hutumiwa kama njia ya kufanya urahisi wa kukariri mawazo fulani. Mfano mmoja wa neno la akrostiki linalotumika sana katika makanisa ya Kiinjili ni neno la kiingereza JOY, ambalo limefafanuliwa hivi: Furaha huja unapomweka Yesu kwanza, Wengine kuwa wa pili, na Wewe mwenyewe kuwa mwisho. [kwa kiingereza: JOY comes when you put Jesus first, Others second, and Yourself last].
3
Ibada
Made with FlippingBook - Share PDF online