Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

8 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Baada ya kutamka/ kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho) sali sala ifuatayo: Njoo Roho Mtakatifu, uzitiae msukumo nafsi zetu, na utuwashe kwa moto wa kiroho, Amina. ~ Rhabanus Maurus (Mtawa wa Kibenedikti wa Kijerumani na Mwalimu wa theolojia ambaye alitambulika sana kwa ukarimu wake kwa maskini. Aliishi mwaka 776 hadi 856 B.K).

Kanuni ya Imani ya Nikea na Sala

Weka kando madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ujibu maswali ya jaribio la Somo la 2, Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu.

Jaribio

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka kutoka kwenye andiko la kipindi kilichopita: Warumi 8:18-21.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko.

3

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za kukusanya

MIFANO YA REJEA

Tazama! Nafanya Kila Kitu Kuwa Kipya!

Moja ya maneno yanayotumika sana katika matangazo ni neno MPYA. Je, unaweza kutaja baadhi ya mifano ya matangazo ya biashara au bidhaa zinazotumia neno hili kuuza bidhaa zao? Kwa nini neno hili ni la kuvutia na lenye nguvu? Maandiko yanafundisha kweli ya msingi kwamba Mungu wetu, anayejulikana kama “Mzee wa Siku” (Dan. 7:9), anahusika kila mara katika upya, kufanya upya, na mambo mapya. Na hii ni kweli hasa kwa kazi zinazohusishwa na Mungu Roho Mtakatifu. Kwa hakika maisha yote ya Kikristo yanaweza kuelezewa kuwa ni kufanywa upya na Roho ili tuweze kuishi maisha yaliyojaa upya ndani ya Kristo. Kama vile Paulo asemavyo katika Warumi 7:6, “Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.” Je, wewe binafsi umepitiaje upya wa uzima ambao Roho Mtakatifu huleta?

1

ukurasa 253  2

Made with FlippingBook - Share PDF online