Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

8 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

njia hiyo hiyo, kuzaliwa upya kunaweza kutokea tu kwa sababu Mungu amechagua kutenda na jambo hili linaweza tu kupokelewa kama zawadi (taz. Yohana 1:12-13; 3:3-8).

b. Mlinganisho wa uumbaji: kama vile pumzi ya Mungu ilivyoingia ndani ya Adamu na kumfanya kuwa nafsi hai, vivyo hivyo wakati wa kuokoka Roho wa Mungu anapulizia tena pumzi yake ya uhai katika uzao wa Adamu na kuwarudishia uhai (2 Kor. 5:17; Gal. 6:15). Kama ambavyo wanadamu hawawajibiki katika mchakato wa uumbaji wao wa kimwili, ndivyo ambavyo pia hawawajibiki katika uumbaji wao wa kiroho.

c. Mstari wa Msingi: Tito 3:4-6

2. Neno na Roho hufanya kazi pamoja ili kukamilisha tendo la kuzaa upya.

3

a. Tunaweza kusema kwamba Neno la Mungu (ambalo kimsingi ni Yesu Kristo, na pia, Injili inayomshuhudia) ni chanzo cha tendo la kuzaa upya kama ambavyo Roho wa Mungu kadhalika ni hanzo cha tendo hilo.

b. Hii ni moja ya kweli kuu ambazo Matengenezo ya Kiprotestanti yalisisitiza kuhusu Roho Mtakatifu. Tunaweza kutofautisha kazi ya Roho katika wokovu lakini hatuwezi kuitenganisha na kazi ya Neno la Mungu.

c. Mistari ya Msingi: (1) 1 Petro 1:23 (2) Yakobo 1:18 (3) Yohana 3:5-6

Made with FlippingBook - Share PDF online