Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 9 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

C. Kanuni muhimu za kitheolojia ambazo Biblia inafundisha kuhusu kufanyika wana:

1. Mungu ndiye Muumba wa watu wote lakini si Baba wa wote.

a. 1 Yohana 3:8 (taz. Yoh. 8:44)

b. Hakuna mwanadamu ambaye kwa asili ni wa familia ya Mungu. Hatukuzaliwa katika familia ya Mungu pale tu tulipozaliwa kimwili kama watoto wachanga, badala yake tunafanyika kuwa wana wa Mungu, kwa kuasiliwa (Efe. 1:5) kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.

c. Mstari wa Msingi: Gal. 3:26.

3

2. Kuwa mtoto wa Mungu sio haki tuwezayo kudai bali ni fursa.

ukurasa 255  6

a. Hatuna madai juu ya Mungu au upendo wake (Mt. 3:9; Rum. 3:10 12; Efe. 2:3).

Dokezo kwa ajili ya Huduma Tendo la kufanywa wana hutusaidia kuelewa kwamba hatuna mamlaka juu ya wokovu wetu. (Unaweza kuchagua marafiki zako lakini sio familia yako). Waongofu wapya hawaji kwa Yesu tu, bali wanakuja katika familia ya Mungu.

b. Upendo na neema ya Mungu ndio sababu pekee ya yeye kutufanya wana. (Rum. 4:16; Rum. 5:20-21; Efe. 2:8-9; Tito 3:4-5).

c. Mistari ya Msingi: (1) Waefeso 2:3-5 (2) 1 Yohana 3:1

Made with FlippingBook - Share PDF online