Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
9 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
3. Kuasiliwa (kufanywa wana) kunatukumbusha kwamba wokovu daima unahusisha kuwa sehemu ya Kanisa la Mungu. Katika uhalisia wake, wokovu unahusisha kuingizwa katika familia mpya ambayo tunaiita Kanisa.
ukurasa 255 7
a. KuasiliwakwetunaMungukunapelekeakubadilikakwautambulisho wa kifamilia. Mtume Paulo anaandika kwamba Kanisa, kwa kweli, ni nyumba ya Mungu (1 Tim. 3:15; Efe. 2:19-20).
Dokezo kwa ajili ya Huduma Kuwa sehemu ya Kanisa kunaleta utofauti. Waongofu
wapya lazima wafundishwe kuthamini muda
b. Watoto walioasiliwa kwa kawaida hutamani kuwa katika nyumba ya Baba yao pamoja na kaka na dada zao (Mdo 2:42; Ebr. 2:11-13; 10:25).
wa kukaa na familia [Kanisa]. Kuwa katika Kanisa ni tofauti na kuwa katika taasisi nyingine yoyote.
c. Mstari ya Msingi : Efe. 2:19-20.
3
4. Kufanywa wana kunatoa njia ya kumkaribia Mungu – kuwa mshiriki wa familia ya Mungu humpa mtu haki na wajibu.
a. Kupitia kufanywa wana tunapata haki ya kumwita Mungu “Abba” (Marko 14:36; Rum. 8:14-17; Rum. 8:29) ambalo ni neno la kibinafsi la karibu kama “baba” au “papa” kwa Kiingereza.
b. Kama watoto tulioasiliwa, Mungu hujidhihirisha mwenyewe kwetu sisi familia yake na kutufunulia mapenzi yake kwa njia ya kipekee, (1 Kor. 2:12-13; Rum. 8:32).
c. Kuadibisha kwa Mungu kunaonyesha nafasi yetu kama wana na binti za Mungu tulioasiliwa kikamilifu (taz. Ebr. 12:5-11).
d. Mstari wa Msingi: Rum. 8:14-18.
Made with FlippingBook - Share PDF online